27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Toronto Raptors mabingwa wapya NBA

CALIFORNIA, MAREKANI

HATIMAYE timu ya kikapu ya Toronto Raptors ya nchini Canada inayoshiriki Ligi ya Kikapu ya NBA nchini Marekani, imetwaa ubingwa wa michuano hiyo msimu huu baada ya kuwafunga wapinzani wao Golden States Warriors vikapu 114-110 jana.

Fainali hiyo ilikuwa ya sita huku Toronto Raptors ikishinda fainali 4-2 na kuifanya timu hiyo iwe bingwa kabla ya kukamilisha mchezo wa saba.

Hii ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi hiyo katika kipindi cha miaka 73, wakiwafunga wapinzani hao ambao walikuwa mabingwa mara mbili mfululizo.

Toronto Raptors ni timu pekee kutoka nchini Canada ambayo inashiriki Ligi ya NBA nchini Marekani, wamechukua ubingwa huo wakiwa kwenye uwanja wa ugenini Oracle Arena.

Mashabiki wa Toronto Raptors, walianza kufanya sherehe za ubingwa huo mapema siku moja kabla ya fainali hiyo ya sita, mitaa ya mjini Toronto mashabiki walikesha wakiimba nyimbo za kuwatakia kila la heri mabingwa hao wapya.

Kitendo hicho ambacho kilifanywa na mashabiki kimetokea kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1993 ambapo mashabiki wa timu ya Baseball, Toronto Blue Jays walipo karibia kutwaa ubingwa wa dunia wa World Series na waliweza kufanya hivyo.

Timu ya Golden States Warriors, walifungwa mchezo huo bila ya kuwa na staa wake ambaye alikuwa anashikilia taji la MVP, Kevin Durant, ambaye aliumia mchezo wa mapema wiki hii katika fainali ya tano. Hata hivyo timu hiyo ilipata pigo lingine kwa staa wake Klay Thompson kuumia goti na kutolewa nje na kuwapa nafasi Toronto Raptors kutwaa ubingwa.

Zikiwa zimesalia sikunde sita mchezo huo kumalizika, Stephen Curry alishindwa kuibeba Golden State huku akikosa pointi tatu ambazo zingeweza kuwapa nafasi za kusonga hadi fainali ya mwisho ya saba.

Kwa upande mwingine nyota wa Toronto Raptors, Kawhi Leonard, ametajwa kuwa mchezaji bora wa fainali hizo na kutwaa tuzo ya MVP baada ya kujikusanyia wastani wa pointi 28.5.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles