23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TOFAUTI KATI YA UJERUMANI, MAREKANI YAZIDI KUTOKOTA

WASHINGTON, MAREKANI


UHUSIANO baina ya Marekani na Ujerumani unazidi kuelekea katika sintofahamu baada ya Rais Donald Trump kwa mara nyingine kutamka kuwa sera ya Ujerumani kuhusu biashara na matumizi ya fedha za kijeshi ni mbaya mno kwa Marekani.

Kufuatia kauli hiyo, wanasiasa waandamizi nchini Ujerumani wanataka Trump apingwe vilivyo.

Matamshi ya Trump yalikuja saa chache tu baada ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kusema mahusiano kati ya nchi hizo yamebadilika kwa kiasi kikubwa baada ya kukosekana maafikiano wakati wa mkutano wa nchi saba zilizoendelea zaidi kiviwanda (G7) wiki iliopita.

"Tunao upungufu mkubwa wa kibiashara na Ujerumani. Isitoshe wanalipa kiwango cha chini mno kuliko kile wanachopaswa kulipa kwa matumizi ya jeshi la Jumuiya ya Kujihami ya Magharibi (NATO).

“Hiyo ni mbaya kwa Marekani. Hilo litabadilika,” huo ni ujumbe ambao Rais Donald Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, kama jibu kwa maneno ya Kansela Merkel, ambaye alizungumzia athari ya msimamo wa utawala wa Marekani kwa uhusiano wake na Ulaya.

Mara kwa mara, Trump ameitaka Ujerumani kutimiza kiwango cha fedha kwa jeshi la NATO ambayo ni asilimia mbili ya pato la jumla la nchi hiyo.

Aidha mara kwa mara Trump hutaja sera ya Merkel ya kuwafungulia milango wakimbizi kuwa kosa linaloweza kusababisha janga.

Mvutano kati ya Marekani na Ujerumani ulijionesha dhahiri wakati wa mkutano wa kilele wa wakuu G-7, uliofanyika Taormina nchini Italia mwishoni mwa wiki iliyopita.

Ni baada ya Trump kutangaza kuwa anahitaji muda zaidi kuamua ikiwa Marekani itajiondoa au itaheshimu mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

Mkataba huo unataka nchi kupunguza utoaji wa gesi chafu zinazosababisha ongezeko la joto duniani.

Baadhi ya wanasiasa wa Ujerumani bila kujali itikadi zao wamejiingiza kwenye mvutano huo wakimpinga Trump miongoni mwao akiwa Waziri wa Mambo ya Nje Sigmer Gabriel ambaye pia ni naibu wa Kansela.

Mwingine ni Kiongozi wa chama cha Social Democratic SDP Martin Schulz atakayeshindana na Merkel katika uchaguzi wa Ujerumani Septemba mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles