24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TMA yatoa tahadhari upepo mkali mikoa mitano, Zanzibar

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya kuwepo upepo mkali na mawimbi makubwa katika baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara na visiwa vya Unguja na Pemba.

Mikoa hiyo ni Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa ya utabiri wa hali ya hewa iliyotolewa juzi na TMA, inaonyesha kutakuwa na upepo mkali sambamba na mawimbi makubwa kwa siku tano yaani kuanzia Agosti 21 hadi 25.

Angalizo hilo la upepo mkali limetolewa pia kwa baadhi ya maeneo ya Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa.

Mamlaka hiyo imewataka watumiaji wa bahari na maeneo yaliyotajwa kuchukua tahadhari.

 “Tahadhari ya upepo mkali na mawimbi makubwa imetolewa kwa maeneo ya ukanda wa pwani yote, katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kulingana na taarifa hiyo, athari zinazoweza kutokea ni matatizo ya usafiri, kuhatarisha maisha kutokana na uwezekano wa boti/meli kuzama, kutawanyishwa/kupeperushwa kwa takataka, kuathirika kwa shughuli za uvuvi na ucheleweshwaji wa usafiri baharini.

Hali hiyo ya upepo mkali ilishuhudiwa jana katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles