TIGO YAZINDUA KAMPENI YA ‘TUMEKUSOMA’

0
23

Na MWADISHI WETU -DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya simu ya Tigo Tanzania, imezindua rasmi kampeni ya Tumekusoma ambayo ni mkakati wa kufikia wateja wake nchi nzima kwa bidhaa na huduma bora zinazoendana na mahitaji yao kwa muda mwafaka.

Kampeni hiyo ya Tumekusoma pia itaendana na uzinduzi wa namba mpya ya huduma ya *147*00#, itakayowezesha wateja wa Tigo kupata huduma mbalimbali za sauti kutoka Tigo kwa hatua rahisi zaidi, ambapo wateja watakaotumia namba hiyo pia watapata bonasi kubwa ya vifurushi na muda wa maongezi kila wanapotumia namba hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jana, Mkurugenzi wa Bidhaa na Huduma za Tigo, David Umoh, alisema Tumekusoma ni hitaji la watumiaji wa mitandao ya simu la menu au namba ya muda ambayo itarahisisha hatua za kununua vifurushi au kufanya miamala ya fedha.

“Menu hii mpya inajibu mahitaji yote, ni rahisi sana kutumia. Pamoja na haya namba mpya ya *147*00# inawapa wateja ofa kabambe ya nyongeza ya muda wa maongezi, sms na data kila mara watakaponunua vifurushi kupitia namba hii,” alisema.

Alisema faida nyingine kubwa ya menu hiyo mpya ni ofa za Chapchap zinazowawezesha wateja kununua muda wa maongezi na vifurushi vinavyoendana na mahitaji na tabia zao za kipeee za matumizi ya simu, jambo ambalo linaendana na lengo la Tigo la kuwaongezea thamani wateja wake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here