23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TIC YAFUNGUA OFISI KANDA YA KUSINI

 

Hadija Omary, Lindi



Taasisi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TOC), imefungua ofisi mkoani Mtwara ili kusogeza huduma za uwekezaji Kanda ya Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonyesho ya Wakulima Nane Nane, yanayofanyika mkoani Lindi, Kaimu Meneja wa Taasisi hiyo, Dotto Stanley amesema sababu iliyowasukuma kufungua kituo hicho cha uwekezaji kwa Kanda ya Kusini ni kusogeza huduma ya uwekezaji kwa wawekezaji na  wajasiriamali.

“Sababu nyingine ni kutambua maeneo yaliyotengwa na halmashauri kwa ajili ya uwekezaji ambayo itasaidia kuwa na kazi data itakayoweza kuwasaidia wawekezaji watakaohitaji kuwekeza katika mikoa hiyo.

“Kituo hicho kitakuwa na dhamana ya kuhudumia mikoa mitatu ya Kanda ya Kusini ikiwamo Lindi, Mtwara na Ruvuma ambapo wawekezaji wote wa mikoa hiyo watapata huduma katika Mkoa wa Mtwara mbapo ofisi za taasisi zimefunguliwa,” amesema.

Aidha, Stanley ameelezea vipaumbele wanavyovizingatia katika kuwavutia wawekezaji kuwekeza katika kanda ya kusini kumezingatia ajenda za nchi ikiwamo viwanda, kilimo na uwepo wa gesi hasa kwa Mkoa wa Mtwara.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shahibu Ndemanga ameipongeza TIC kwa kufungua kituo hicho na kuongeza kuwa ujio wa taasisi hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuitangaza mikoa wa kusini katika uwekezaji.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles