31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

THBUB yashauriwa kuelimisha wananchi haki ardhi

Mwandishi Wetu-Lindi

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeshauriwa kujikita katika kutoa elimu ya haki ya ardhi na mirathi kwa kuwa maeneo hayo yameonekana kuwa na changamoto kubwa kwa jamii nchini.

Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alipokutana na ujumbe wa THBUB na viongozi wa asasi ya kiraia ya Haki Maendeleo walipomtembelea ofisini kwake kumpa pole kufuatia maafa waliyoyapata yaliyosababishwa na mafuriko ya mvua yaliyotokea mkoani humo hivi karibuni.

Zambi akiongea katika kikao hicho kilichofanyika mwishoni mwiki mjini hapa, alisema kuwa tume iwaelimishe wananchi kuhusu haki zao ili wazijue na waeleweshwe taratibu za kufuata pindi wanapotaka kudai haki zao zitakapokuwa zimevunjwa.

Alisema kuwa shida ipo kwa wananchi wa chini ambao kwa kiasi kikubwa hawajui haki zao na hata ikitokea kuwa wanazifahamu, bado hawajui njia sahihi za kufuata pale haki yake inapokuwa imevunjwa ili kuidai.

“Kwenye mirathi huko kuna matatizo, watu hawajui haki zao, ardhi pia kuna shida sana, lakini wananchi hawajui njia za kufuata kudai haki zao, tuwasaidie wananchi hawa ili wajue njia za kufuata kudai haki zao.

 “Mheshimiwa Rais Magufuli anatuambia kila siku kuwa ametutuma ili tukatatue kero za wananchi, tena wananchi wa chini. Tunatambua kuwa tume hamuwezi kwenda kila mahali, sisi tupo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi kutatua kero zao, hivyo tushirikiane katika kutatua kero hizo,” alisema Zambi.

Kwa upande wake, Kamishna wa THBUB, Amina Talib Ali, alimweleza mkuu wa mkoa kuwa tume imekuwa ikifanya kazi zake kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo za Serikali, binafsi na taasisi za kimataifa katika kuhakikisha haki za binadamu na misingi ya utawala bora inalindwa na kukuzwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles