33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TFS yahofia miti ya mpingo, mninga kutoweka nchini

Mwandishi Wetu

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), umesema kuna tishio la miti bora ya asili ya mpingo, mninga, mkongo na mvule kutoweka nchini ambapo tayari wamechukua hatua mbalimbali kuhakikisha miti hiyo inaendelea kuwepo.

Akizungumza leo Jumapili Machi 17, jijini Dar es Salaam, Meneja wa Kituo cha Uzalishaji Mbegu za Miti wa TFS mkoani Morogoro, Dk. Hamza Katety amesema kwa sasa wanapotafuta miti hiyo hata mahali ambako waliamini ipo wanaikosa.

“Kuna miti tuliyozoea kuiona katika nchi yetu na sasa imeanza kupotea, miti hiyo maarufu imekuwa adimu kuipata na hata ikipatikana haiko kwenye ubora unaostahili.

“Hatua ambazo TFS tunachukua ni kuhifadhi mbegu bora za miti hiyo, tuna mashamba ya mbegu bora ambayo yameanzishwa, tayari miti ya mvule, mkongo na mkangazi imepandwa katika vishamba vidogo,” amesema Dk. Katety.

Ametoa rai kwa Watanzania kuhakikisha wanashiriki kuitunza miti hiyo ambayo ni alama nchini na huenda ni mpango wa Mungu kwa kuweika katika ardhi ya Tanzania.

Akizungumzia mbegu bora, Dk. Katety amesema kupitia Kituo cha uzalishaji wa mbegu za miti Morogoro ambacho kipo chini ya TFS Wizara ya Maliasili na Utalii kitaendelea kuzalisha mbegu bora na kushauri ni vema wananchi wakapa ushauri kabla ya kununua mbegu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles