31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TFS yafunga mtambo wa kuchakata asali Manyoni

Mwandishi Wetu

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), imefunga mtambo wa kuchakata mazao ya nyuki wilayani Manyoni mkoani Singida wenye uwezo wa kuchakata asali lita 500 kwa siku.

Mtambo huo uliogharimu Sh milioni 80, unatarajiwa kuondoa tatizo la ubora duni wa asali na nta katika ukanda huo na maeneo ya jirani.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino wa TFS, Tulizo Kilaga amesema mtambo huo umefungwa katika kiwanda chao lakini pia wafugaji wa nje wataruhusiwa kuchakata mazao yao.

“Kiwanda kwa kiasi kikubwa kitategemea malighafi toka kwenye misitu uliopo Itigi na katika uvunaji wa awali tumefanikiwa kuvuna mizinga 459 kati ya 729 na kupata asali kilogramu 6,175 sawa na tani 6.175 wastani kilo 13.45 kwa mzinga,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles