tff yasaka mbunifu wa nembo ya afcon

0
1071

Na Elizabeth Joachim

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza shindano kwa wabunifu wa watakaoweza kubuni Nembo maalumu (Mascot) itakayotumika katika fainali za vijana U17 zitakazofanyika mwakani nchini Tanzania.

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Septemba 24 na afisa habari na mawasiliano wa shirikisho hilo, Clifford Ndimbo amesema wabunifu watakaofanya vizuri katika zoezi hilo la ubunifu wataitwa kwa hatua inayofuata.

Ndimbo ameeleza kwamba zoezi hilo litadumu kwa siku nane na litadumu hadi Octoba 1 mwaka huu na washiriki wanatakiwa kuambatanisha kazi zao za kibunifu kwa njia ya barua pepe kupitia email; tanfootball@tff.or.tz.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya vijana chini ya umri wa miaka 17 yatakayofanyika nchini kupitia Uwanja wa Taifa na Chamazi Coplex.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here