27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TEF kufungua maombi ya ujasiriamali Januari 2020

MWANDISHI MAALUMU-NIGERIA

TAASISI ya Tony Elumelu Foundation (TEF) inayoongoza barani Afrika, iliyowekwa katika kuwezesha wafanyabiashara wa Afrika, imetangaza kuanza kupokea maombi ya wajasiriamali kwa mwaka 2020 chini ya Mpango wa Ujasiriamali wa TEF, Januari 1, 2020.


Maombi hayo, waombaji wataomba kupitia TEFConnect, kitovu cha mtandao wa dijiti kwa ikolojia ya ujasiriamali wa Kiafrika, iliyoundwa na taasisi hiyo.
Mpango wa ujasiriamali wa TEF uko wazi kwa wajasiriamali kutoka Afrika nzima, ambao hulazimika kuwa na maoni mapya ya biashara au biashara zilizopo chini ya miaka mitatu zinazofanya kazi katika sekta yoyote.


Waombaji waliofanikiwa watajiunga na wanufaika zaidi ya 9,000 wa sasa kutoka nchi 54 za Afrika, na watapata mafunzo ya biashara, ushauri, pesa isiyolipwa ya pauni 5,000 ya mtaji wa mbegu na fursa za mitandaoni.


Mwaka jana, taasisi hiyo ilipokea maombi takriban 216,000 na asilimia 42 wakiwa ni wajasiriamali wanawake kutoka kila nchi barani Afrika.
Programu hiyo ni ahadi ya miaka 10, dola milioni 100 kujitolea kubaini, kutoa mafunzo, ushauri na kufadhili wafanyabiashara vijana wa Afrika 10,000.


Lengo ni kuibua mamilioni ya ajira na mapato yanayotakiwa kwa maendeleo endelevu ya bara hilo, kutekeleza falsafa ya Africapitalism, ambayo inachukua nafasi ya sekta binafsi kama injini ya ukuaji kwa Afrika na inasisitiza umuhimu wa kuunda utajiri wa kijamii na kiuchumi.


Kwa mujibu wa ripoti ya athari ya msingi ya 2018, asilimia 70 ya idadi ya biashara katika mtandao wake wa alumni ilikuwa bado inafanya kazi miaka miwili baada ya kufaidika na programu hiyo.


Ripoti hiyo pia ilibaini ongezeko la mapato la asilimia 189 yanayotokana na kuongezeka kwa asilimia 197 kwa idadi ya kazi za ziada zinazoundwa na walengwa baada ya kuhitimu kutoka programu hiyo, na pia kujitolea kwa asilimia 100 kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles