TCRA YAPIGILIA MSUMARI SAKATA LA VISIMBUZI

0
972

Na MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAMMkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), James Kilaba, amesema kulipisha maudhui yanayotazamwa bila kulipia (FTA) ni kwenda kinyume na kanuni na sheria za utangazaji zilizopo.

Amesema kufanya hivyo kunawanyima Watanzania wengi wenye vipato vya chini na kati wanaotegemea mfumo huo kupata taarifa za habari na matukio mbalimbali.

Hayo aliyasema juzi jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa semina ya wahariri wa vyombo vya habari kuhusu huduma za utangazaji wa maudhui yanayotazamwa bila kulipia.

Alisisitiza kuwa kulipisha maudhui hayo si sahihi.

Alisema maelekezo yaliyotolewa kwa watoa huduma wa visimbusi vya Azam, Dstv na Zuku yaliangalia masilahi mapana ya taifa, ikiwa ni pamoja na kumlinda mlaji wa mwisho.

“Tukumbuke kuwa kama TCRA ingeachia hali kuendelea, watoa huduma hawa wangerasimisha huduma hii kwenye majukwaa yao na kuanza kupandisha bei taratibu kama wanavyotaka kwa sababu ya kurasimisha huduma hii ya kutazamwa bila kulipia na hatimaye wananchi wengi wangeshindwa kumudu tozo za kila mwezi,’’ alisema Kilaba.

Alisema sheria na masharti ya leseni kwa watoa huduma za utangazaji yana malengo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa kupitia maudhui ya wenye leseni za FTA.

Pia FTA kutumia miundombinu ya utangazaji iliyosimikwa nchini badala ya miundombinu tegemezi pamoja na kuwa na miundombinu ya utangazaji imara na endelevu yenye kutoa huduma za utangazaji kwa wananchi wote bila ubaguzi.

“Kujenga mazingira mazuri ya ushindani na kulinda uwekezaji wa hapa nchini kwenye sekta ya utangazaji wa dijitali iliyosimikwa nchini, kupunguza wigo wa mtandao wa ufikishaji wa huduma za utangazaji kwenye maeneo mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here