23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TBS yapewa bil 5/- kuzuia bidhaa feki

Joseph Masikitiko
Joseph Masikitiko

Na Harrieth Mandari, Dar es Salaam

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limepata msaada wa Sh bilioni 6.3 kutoka TMEA kwa ajili ya uboreshaji uhakiki wa viwango vya bidhaa ili kuchochea biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Joseph Masikitiko, alisema katika dunia ya sasa utandawazi ambao unakwenda sambamba na uwepo wa soko huria ni moja ya changamoto kwa taifa katika kuhakikisha kunakuwepo na bidhaa.

“Bidhaa zisizo na ubora haziwezi kushindana katika masoko ya kimataifa na hata ya ndani kwa kuwa zitashindwa kwa  ubora na bidhaa zinazoingizwa nchini,” alisema.

Alisema kupitia mradi huo wa miaka mitatu, TBS itaelekeza zaidi kipaumbele katika kutoa elimu ya ubora wa bidhaa kwa wajasiriamali, kuboresha miundombinu ya Tehama, kusaidia uandaaji sera ya ubora, kuboresha miundombinu ya maabara za kemia na ugezi na pia kuoanisha viwango vya Afrika Mashariki (EAS).

Kwa upande wa changamoto zinazolikabili shirika hilo, Masikitiko alisema limekuwa likikumbwa na changamoto ya miundombinu ya viwango na uhakiki.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolph Mkenda, alisema Serikali itakuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa shirika hilo linawezeshwa ili liweze kufanya majukumu yake kwa ufanisi.

“Sasa hivi ipo fursa kwa wajasiriamali wadogo wadogo ambapo baada ya kuhakikiwa bidhaa zao na kuonekana zinakidhi viwango wanapatiwa alama ya TBS bila malipo kwa hiyo ni vyema wakachangamkia fursa hiyo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles