30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TBA YAWAFIKIRIA WASTAAFU

Na FERDNANDA MBAMILA-

DAR ES SALAAM

WAKALA  wa Majengo nchini (TBA), wamedhamiria  kutoa  kipaumbele cha kuwauzia  nyumba  watumishi  wa umma waliokaribia kustaafu kwa lengo la kuwapunguzia gharama ya maisha pindi watakapostaafu kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana  jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea mradi  wa nyumba za wananchi Bunju, Mtendaji Mkuu wa wakala hao, Elius Mwakalinga,  alisema dhamira  kuu ya mradi huo ni  kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini ili waweze kunufaika  na nyumba za gharama nafuu.

Alisema licha ya kutoa kipaumbele kwa  wananchi wa kipato cha chini  katika  kiwango cha uuzaji wa nyumba, pia wakala hao wanasimamia na kuiendeleza miradi  mbalimbali, ikiwamo ya Serikali na taasisi zake.

“Mwakalinga aliongeza kuwa, kutokana na ongezeko la miradi mingi, hadi sasa mamlaka hiyo imeongeza wataalamu zaidi ya 200 ambao  wana uwezo  mkubwa wa   kujenga  na kusimamia miradi ya majengo mbalimbali,” alisema Mwakalinga.

Alisema katika mradi wa Bunju ambao  unajenga nyumba zaidi ya 1,000, kutakuwa  na huduma zote za kijamii.

“Ndani ya miaka mitano TBA huwa inajenga nyumba zipatazo 10,000, ambapo  kwa kila mwaka hujenga nyumba 2000  kwa Tanzania nzima,” alisema Mwakalinga.
Naye mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Japheth Asunga, aliipongeza Serikali na Wakala wa Majengo nchini, TBA, kwa  kubuni mradi  wa aina hiyo ambao  umekuwa ukiwaletea manufaa wananchi wa kipato cha chini.

Alisema kutokana na jitihada za ujenzi wa majengo za TBA, Serikali ina jukumu la  kusogeza huduma za kijamii kwa haraka ili wananchi watakaokuwa na uwezo wa kuishi maeneo hayo waweze kunufaika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles