31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Taus Likokola: Tanzania hakuna soko la vitabu  

TAUS-LIKOKOLANA GLORY MLAY

KATI ya watu wanaoiwakilisha Tanzania vizuri kimataifa ni mwanamitindo, Tausi Likokola ambaye kupitia ubunifu wake katika mitindo amefanikiwa kufanyakazi na wabunifu mashuhuri duniani akiwemo Gucci , Christian Dior, Tommy Hilfiger, Issey Miyake na Escada.  Mafanikio hayo aliyoyapata kwa sasa anayatumia kutoa elimu ya afya na mitindo kwa wasichana kupitia asasi yake isiyo ya kiserikali ya Tausi Ukimwi Duniani (TAF), inajishughulisha kuboresha elimu na afya kwa watoto yeye akiwa ndiye mwanzilishi na rais wa asasi hiyo.

Tausi pia ni mwandishi wa Sanaa na Afya kupitia kupitia kipawa hicho ameandika mambo mengi katika vitabu vyake vya ‘The Princess African’, ‘Beautiful You’, ‘The Art of Beauty & Health’ na ‘Touch ya Angel’.  Mwanamitindo huyo alizungumza na MTANZANIA na mazungumzo yake yalikuwa kama ifuatavyo.

 

BINGWA: Wewe kama mwandishi wa vitabu unahisi kwanini watanzani wengi hawapendi kusoma vitabu

 

Tausi: Watanzania wengi bado hawajapata elimu ya kutosha juu ya usomaji wa vitabu, ukisoma vitabu unapata maarifa mengi na pia utapata vya kujifunza kutokana na maisha yetu yanavyokwenda kila siku.

“Katika safari zangu zote huwezi ukaenda sehemu ukakuta Mtanzani anasoma vitabu yeye anakuwa anaangalia ‘move’ na kuchati sana kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook na mitandao mingine wanakuwa wanapoteza muda wakati wangesoma vitabu wangepata maarifa mapya”

 

Mtanzania: Nini kilikusukuma ukaandika vitabu?

 Tausi: Mimi wakati nasoma sekondari nilikuwa na ndoto ya kuandika kuliko kuongea kwa hiyo naona uzoefu ulianzia huko kwa sababu tulipokuwa tukijadiliana baada ya muda nilikuwa nikiyaandika katika karatasi hapo nikaamini kuwa naweza kuandika.

 Mtanzania:Umeshaandika vitabu vingapi hadi sasa?

 Tausi: Mpaka sasa nimefanikiwa kuandika vitabu Vinne vya urembo na ujasiriamali; ‘The Art of Beauty & Health’, ‘The African Princess’, ‘Beautiful YOU’ na  ‘The Touch of an Angel’

Mtanzania: Kuna tofauti gani ya soko la vitabu hapa Tanzania na nchi nyingine kama Marekani?

Tausi: Katika nchi yangu soko hakuna kutokana na watu hawapendi kusoma vitabu wanapoteza muda wao mwingi katika kusoma magazeti na kuangalia move lakini kushika kitabu na kusoma ni mwiko ni tofauti na wenzetu kule soko ni  kubwa kutokana na watu wengi wakubwa na wadogo wanapenda kusoma vitabu wapo radhi kulala mchana kutwa kuliko kusoma kitabu.

 Mtanzania: Waandikaji vitabu ni wengi ila wasomaji ni wachache utafanyaje hadi watu wapende kusoma vitabu?

 Tausi: Kweli watu wengi hapa Tanzania wapo radhi kufuatilia maisha ya mtu kuliko kusoma vitabu,kusoma kitabu hakikuongezei maarifa peke yake pia itakusaidia kujua safari za watu mbalimbali walizopitia katika maisha yao.

 Mtanzania: Mbali na uandishi unawasaidiaje wasichana wa Tanzania wanaotaka kuwa kama wewe?

Tausi: Nimeanzisha mradi wangu ya Tausi Likokola Modal Search ambao unashugulika na kutafuta warembo   mikoani, tunawafundisha kila kitu jinsi ya kujitunza kwenye urembo, mazoezi na vitu vingine vingi.

Mtanzania:Na kwawale ambao wamesha kata tamaa kuwa hawaweziunawambia nini?

Tausi:Wanachotakiwa kupeana ushirikino kwa sababu kila mtu kaumbwa kwa tofauti yake kwa hiyo kila mtu ana nafasi yake na kuwa na malengo yake lakini pale mnapopeana ushirikiano kila kitu kinakuwa sawa.

 Mtanzania:Kuna baadhi yao wanasema kwamba ukishakuwa na mtoto urembo unakuwa umekwisha kama wewe unalizungumziaje?

 Tausi:Mazoezi ni kitu kikubwa sana katika maisaha  ya mwanadamu kwa hiyo ukizingatia mazoezi urembo wako utabaki kuwa pale pale, atakama unawatoto ukifanya mazoezi urembo wako unabaki pale pale wazingatie mazoezi na vyakuwa wanavyokula  kwa sababu vinachangia kuwa na muonekano mbaya kwa kuwa vinaongeza mafuta mengi mwilini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles