31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TATIZO LA WALIMU WA SAYANSI KUTATULIWA KUFIKIA 2020/21

NA RAMADHAN HASSAN, Dodoma


SERIKALI imesema imejipanga kuhakikisha inamaliza tatizo la upungufu wa walimu wa sayansi nchini  kufikia mwaka 2020/2021.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Kakunda alitoa kauli hiyo  bungeni jana  alipojibu swali la nyongeza la Mbunge wa Magu, Boniventure Kiswaga (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua mpango wa serikali wa kuhakikisha inamaliza changamoto ya  walimu wa sayansi.

Akijibu swali hilo, Kakunda alisema kwa sasa kuna upungufu wa walimu 19,000 nchini.

Ili kukabiliana na upungufu huo, Naibu Waziri  alisema, serikali inaandaa utaratibu wa kuajiri walimu wa sayansi 6,000 mpaka kufikia mwishoni mwa Juni mwaka huu.

Katika swali la msingi, Mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kupeleka walimu Magu.

Alisema  mwaka 2014/15 jimbo hilo halikupatiwa walimu wa shule za msingi na bado kuna uhaba wa walimu.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri  alisema Halmashauri ya wilaya ya Magu ina walimu wa shule za msingi 1,281 kati ya walimu 2,002 wanaohitajika hivyo kuna upungufu wa walimu 821.

Kakunda  alisema kati ya walimu 1,276 wa shule za msingi walioajiriwa  Desemba mwaka jana, Halmashauri ya Wilaya ya Magu ilipangiwa walimu 56 ambao wameripoti kwenye shule zilizokuwa na mahitaji makubwa.

“Walimu 77 ambao ni miongoni mwa walimu wa ziada wa masomo ya sanaa katika shule za sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Magu wamehamishiwa shule ya msingi,”alisema

Pia alisema katika mwaka wa fedha 2017/18 serikali imepanga kuajiri walimu 10,130 wa shule za msingi nchi nzima   kukabiliana na uhaba wa walimu katika maeneo mbalimbali.

Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Viti maalumu, Cecilia Paresso (Chadema) alitaka kujua mkakati wa serikali wa kuajiri watumishi wa afya na elimui kufikia angalau asilimia 60 au 70.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri   alisema serikali kwa mwaka wa fedha 2017/18 imejianga kuajiri watumishi 52,000 ambao kati yao 33,000 ni watumishi wa afya na walimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles