30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TANZANIA YAONGOZA KUSHTAKIWA AFRIKA

Na ELIYA MBONEA – ARUSHA


SERIKALI ya Tanzania inaongoza kwa kushtakiwa katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (AfCHPR).

Mahakama hiyo ina kesi 180 ambapo kati ya hizo 117 zimefunguliwa dhidi ya Serikali huku 94 kati ya 117 zikiwa zimefunguliwa na wafungwa na mahabusu waliopo magereza.

Hayo yalielezwa hivi karibuni baada ya kikao kilichowakutanisha Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Julius Mashamba, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali,

Dk. Ally Possi pamoja na Msajili wa Mahakama ya Afrika, Dk. Robert Eno, waliokutana mjini hapa.

Akizungumza baada ya kufanyika majadiliano ya kina, Wakili Mkuu wa Serikali, Dk. Mashamba, alisema ofisi yake iliona haja ya kutembelea mahakama hiyo mbali ya kujifunza lakini pia kuona uendeshaji wa shughuli zake.

“Kwa taarifa walizotupatia hadi sasa Tanzania ndiyo nchi inayoongoza kwa kushtakiwa ikiwa na kesi 117. Tumegundua wengi walioishtaki Serikali kuhusu haki zao ni watu waliopo gerezani au mahabusu,” alisema Dk. Mashamba na kuongeza:

“Wanalalamikia haki zao katika kesi za jinai hazijatekelezwa kwa namna kesi zilivyosikilizwa au kuchelewa kupata nakala za mwenendo wa kesi ili wakate rufaa au kunyimwa msaada wa sheria,” alisema.

Katika hilo, Dk. Mashamba, alisema wamejaribu kuieleza Mahakama ya Afrika nia ya Serikali ya kutaka kuona haki za kila mtu zinalindwa na

pale wananchi wanapoona haja ya kwenda mahamakani basi Serikali pia ipate fursa ya kujitetea.

Alisema jambo kubwa lililowafanya pia watembelee mahakama hiyo ni wingi wa kesi hizo na hasa zikichukuliwa kuwa zimekuwa zikifanana kwani wengi hudai kutopata msaada wa kisheria wakati mahakama za ndani zilishatoa uamuzi wake.

“Tumezungumza nao yale mambo ambayo tayari yalishaamriwa na mahakama kama msaada wa sheria, nakala za hukumu kuchelewa basi tukae nao kujadili kabla hawajalifikisha mbali ili Serikali ilifanyie kazi.

“Kuna mambo pia tumeyaona yanahitaji kufanyiwa kazi kwa pamoja, kwanza ni kuwajengea uwezo watendaji wa Serikali hususani idara zinazoshtakiwa zaidi. Tufanye mafunzo ya pamoja.

“Mfano kesi nyingi zinatoka gerezani, labda tukae na watu wa magereza, mahakama, polisi na waendesha mashtaka tuangalie tunawezaje

kuwajengea uwezo na kuwapa mafunzo ya haki za binadamu na namna gani mahakama hii inafanya kazi,” alisema.

Anazitaja sababu zinazochangia watu kufungua kesi mahakama hiyo ni pamoja na mkataba wa uanzishwaji wake na kuridhia vigezo vinavyoelekeza ili mtu afungue kesi lazima nchi yake iwe imetoa idhini kwa watu wake zikiwamo asasi za kiraia kuishtaki.

Inaendelea………………….. Jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

 

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Nilisikiliza Mzee Sumaye akizungumzia kuiondoa CCM Madarakani. Kwa kweli hotuba yake haina mvuto wala ushawishi ukilinganisha na hotuba za wazungumzaji wengine. Chadema ilishafanya makosa kuwakaribisha viongozi waliokosa madaraka CCM. Viongozi kma Sumaye na Lowasa walishakuwa serikalini kwamuda mrefu sana na hawakuwa wanaharakati au watuwaliojipambanua kutaka demokrsia ya kweli Tanzania, Wanachotaka ni Urais ndiyo maana leo wananzungumzia “demokrasia ya kweli”. Vyama vya upinzani ni vema vikaachana na viongozi hawa. Vijijenge upya kwa kuwatumia viongozi wao (aina ya Slaa). wapo wengi. Zito, Mbowe, Mdee, Lisu NK. Kwa matazamo wangu, hawa hawatafuti Urais bali mabadiliko ya kweli. Sumaye na Lowasa wana mtazamo finyu sana. Urais au kulinda mali zao

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles