23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania mwenyeji wa jukwaa la vitambulisho

Na Aziza Masoud, Dar es Salaam

ZAIDI ya nchi 25  zinakutana nchini katika mkutano wa Jukwaa la Vitambulisho vya Elektroniki Afrika unaotarajia kuanza   Dar es Salaam leo.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine utajadili changamoto zilizopo katika masuala ya uandikishaji  na kutafuta njia za kuzitatua.

Mkutano huo wa kwanza kufanyika katika   Afrika unatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mathias Chikawe na kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki 300 kutoka nje ya nchi.

Akizungumza kwa  niaba ya Mkurugenzi Mkuu Mamlaka  ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu, Mkurugenzi wa Mfumo wa Kompyuta,  Joseph Makani,   alisema  mkutano huo wa siku tatu utahusisha nchi ambazo zinatumia Mfumo wa Vitambulisho vya Taifa.

“Kutakuwa na watoa mada kuhusu vitambulisho  kutoka nchi mbalimbali duniani ambao wataeleza  uzoefu wao katika mataifa wanayotoka.  Kila nchi ina changamoto zake kutokana na inavyojiendesha… kupitia mkutano huu tutabadilishana mawazo na kushaurina jinsi ya kukabiliana nazo,”alisema Makani.

Alisema mkutano pia utaisaidia Tanzania kujua nchi wanazotumia Vitambulisho vya Taifa kwa sasa wamefika wapi katika uchumi na wamefaidika nini baada ya kuvitumia katika kutolea huduma mbalimbali za taifa na jamii.

Nchi zitakazoshiriki ni pamoja na Ghana, Rwanda, Botswana, Burundi, Malawi, Zambia, Uganda, Kenya, Djibout, Namibia, India, Mali, Estonia, Zimbabwe, Magascar na Liberia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles