31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania kupata msaada wa Sh trilioni 1.4 kusaidia sekta ya afya

Mwandishi wetu -Dodoma

SERIKALI itanufaika na msaada wa dola za Marekani milioni 600 (Sh Trilioni 1.4) zitakazotolewa na Taasisi ya Global Fund Januari mwakani kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na Ukimwi, kifua kikuu na malaria katika  kipindi cha miaka mitatu.

Ahadi hiyo ilitolewa jijini Dodoma na Mkuu wa Mfuko huo Barani Afrika, Linden Morrison, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango.

Alisema fedha hizo zitatumika kuimarisha afya kwa kupambana na maradhi hayo ambapo vifaa tiba na vitendanishi  vitanunuliwa kupitia msaada huo katika kipindi cha miaka mitatu (2021-2023).

Alisema katika kipindi cha miaka 15 ambacho taasisi yake imekuwa na uhusiano mzuri na Tanzania, mfuko wake umetoa msaada wa dola za Marekani bilioni mbili kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya hususan katika mapambano dhidi ya Ukimwi, kifua kikuu na Malaria.

 Dk. Mpango kwa upande wake aliishukuru taasisi hiyo ya kwa mchango iliyoipatia Tanzania katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo hasa malaria, ugonjwa unaoongoza kusababisha vifo vya Watanzania.

Dk Mpango aliahidi fedha hizo zitatumika ilivyokusudiwa ili zilete matokeo chanya kwa kuwafikia walengwa nchini kote.

 ‘‘Nimefurahi kwa sababu nina matumaini kuwa tumepata nguvu ya kupambana na magonjwa haya makubwa, ili Watanzania wawe na afya njema na waweze kujenga uchumi wa nchi yao,’’ Alisema Dk Mpango.

Aidha Dk Mpango alisema katika kikao hicho wamejadili namna ya kuboresha ushirikiano uliopo kati ya pande hizo mbili ikiwemo kuangalia namna ya kutoa msamaha wa kodi kwenye vifaa yakiwemo magari ya kubebea wagonjwa na dawa zinazoingizwa nchini na taasisi hiyo kwa ajili ya mradi huo.

“Ili kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Global Fund, nchi itahakikisha inakuwa na ushiriki mpana katika bodi ya wakurugenzi ya mfuko huo ili sauti ya nchi iweze kusikika zaidi,” alisema Dk Mpango.

Kuhusu ubadhirifu wa zaidi ya dola za Marekani 400,000 zinazodaiwa kufujwa na baadhi ya watendaji wa Serikali wanaotekeleza mradi huo nchini, Dk. Mpango aliahidi kwamba Serikali itachunguza na kuwachukulia hatua kali wote waliohusika na vitendo hivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles