27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania ina upungufu wa madaktari 91%

sittaNa Elias Msuya, Dodoma

TANZANIA inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi wa afya, hali inayochangia vifo kwa wagonjwa wengi kutokana na kukosa huduma.

Akiwasilisha mkakati wa kuboresha rasilimali watu katika sekta ya afya nchini, kwa wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii na Maendeleo ya Jamii, Meneja wa Mipango na Utetezi wa Sera  kutoka Taasisi ya Benjamin Mkapa, Manka Kway, alisema mwaka 2014-15 kulikuwa  na mahitaji ya madaktari wasaidizi 1,744, lakini waliopatikana ni 149 tu.

Alisema tathmini hiyo imefanyika wilaya 30 za mikoa saba ya Tanzania ambayo ni Geita (Bukombe na Chato), Iringa (Kilolo, Mafinga, Iringa, Mufindi), Kilimanjaro (Mwanga, Siha, Rombo, Hai, Moshi na Moshi Manispaa).

Mikoa mingine ni Mtwara (Tandahimba, Masasi, Mtwara, Manispaa ya Mtwara), Pwani (Kisarawe, Rufiji, Bagamoyo, Kibaha na Mji wa Kibaha), Ruvuma (Mbinga, Namtumbo, Songea na Mji wa Songea), Shinyanga (Shinyanga Manispaa na Halmashauri ya Shinyanga).

“Mahitaji ya madaktari wasaidizi kwa mwaka 2014-15 yalikuwa 1,744, waliokuwapo ni 149 na waliopungua 1,595 sawa na asilimia 91,” alisema Kway.

Mbali na madaktari wasaidizi, alisema kuna upungufu wa maofisa wauguzi kwa asilimia 33, maofisa tabibu wasaidizi kwa asilimia 78, maofisa tabibu kwa asilimia 26, wauguzi kwa asilimia 72, maofisa wauguzi kwa asilimia 53 na wataalamu wa maabara kwa asilimia 37.

“Sekta ya afya inakabiliwa na uhaba wa rasilimali watu kwa asilimia 52 kupitia ikama ya mwaka 2014…zaidi ya asilimia 74 ya madaktari waliopo wanafanya kazi maeneo ya mijini… wakati daktari mmoja anahudumia wagonjwa 78,880 maeneo ya vijijini, daktari mmoja mijini anahudumia wagonjwa 9,095. Shirika la Afya Duniani (WHO) linaelekeza uwiano wa 1:10,000,” alisema Kway.

Baadhi ya wabunge wakichangia maoni kuhusu tathmini hiyo, waliitaka Serikali kurekebisha sera na sheria zake ili kuweka mazingira wezeshi kwa watumishi wa afya kufanya kazi vijijini.

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), alisema sera ya afya inayowezesha madaktari wa mijini kulipwa zaidi ya wanaofanya kazi vijijini ni kikwazo kwao kwenda vijijini.

“Kwanini mhitimu wa shahada ya udaktari akiajiriwa Hospitali ya Taifa Muhimbili au Mwananyamala analipwa mshahara mkubwa kuliko yule anayefanya kazi Wilaya ya Nzega?” alihoji Bashe.

Alisema tatizo hata bajeti ya afya inapopitishwa bungeni huwa haifikishwi yote, hivyo akawataka wabunge kusimamia bajeti hiyo itolewe kikamilifu.

Naye Mbunge wa Urambo Mashariki, Margaret Sitta, alisema ili watumishi wa afya waende vijijini ni vema wapewe mafao ya kuwa huko.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles