TANZANIA  BADO  KUFAIDIKA NA UVUVI BAHARI KUU

0
34

Na  Mwandishi Wetu


SEKTA  ya  uvuvi nchini na haswa uvuvi wa bahari kuu ni  bado sana kimapato na kitija kwani hakuna cha kueleza wala kuonesha kwa mhitaji maelezo.

Ukifika kwenye kile kinachoitwa Soko la Kimataifa la Samaki Feri utakachoona na kuambulia ni shombo na visamaki viisivyo haja.

Wale samaki wanaokataliwa na mataifa mengine ndio watu wetu wana kula kwani samaki bora hatuna uwezo kwa bei  kwa watu wa kawaida kwani ghali sana.

Isitoshe wavuvi wetu hawana uwezo wa kwenda kuvua bahari kuu na kama wakipatikana samaki wanauzwa huko moja kwa moja na nchi kukosa mauzo hayo kwani yanainingia mifuko ya watu binafsi.

Udanganyifu unaonekana kushamiri kwenye uvuvi kuliko sehemu nyingine isipokuwa dhahabu kutokana na utendaji kazi na mazingira yake.

Sio hoja pale Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga  Mpina, alipolalama kuwa kwa nini hakuna maendeleo ya sekta ya uvuvi baharini  wakati tunayo ukanda wa pwani wa bahari wa zaidi ya kilomita 1405 kutoka Tanga hadi Mtwara!

Mpina aliwataka wafanyakazi wa wizara yake wawe na mipango thabiti ya kuongeza pato la taifa kutokana na sekta ya uvuvi.

Wawekezaji  wameanza  kuja kuvua nchini mwetu kihalali kwani  Meli mbili za uvuvi za Kampuni ya Simon and Zam Shipping Agent kutoka Taiwan zilitia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam na kushusha samaki tani nne katika gati namba sita ambao  inadaiwa  kuwa wangeuzwa katika soko la Kimataifa la Samaki Feri lililoko Manispaa ya Ilala lakini haikuwa  hivyo na badala yake walienda kuuzwa Zanzibar  na ikaamuliwa kuwa ni Tanzania Maritime Deepsea Authority (TMA) yenye makao makuu yake Zanzibar.

Waziri  wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba  wa wakati huo alizipokea meli hizo Dar es Salaam na kusema samaki hao wamevuliwa kwenye bahari kuu (EEZ), tayari wamenunuliwa na kampuni ya Lucky Fishing ya Dar es Salaam wakiwa ni mchanganyiko wa aina mbalimbali wakiwemo wa jamii ya samaki pendwa , jodari.

Alisema kulingana na kanuni Namba 10 ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari kuu ya mwaka 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2016 inampasa mmiliki wa meli ambaye anaomba leseni kwa ajili ya kuvua katika ukanda wa uchumi wa bahari ya Tanzania kuleta meli yake katika bandari za Tanzania.

Lengo ni ukaguzi wa awali kabla ya kupata leseni na kushusha samaki (fish landing )wasiolengwa baada ya kuvua.

Alizitaja bandari zitakazohusika kuwa ni pamoja na bandari ya Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga na Mtwara.

Meli zilizoshusha samaki  kwa ajili ya majaribio ili kuona jinsi Bandari ya Dar es Salaam inawezaje kuhudumia meli hizo za uvuvi kwa lengo la kubaini maeneo ya kufanya maboresho husika kwenye  gati hiyo na baadaye kufanyiwa ukaguzi wa meli kulingana na vigezo husika kwa uvuvi.

Dk Tizeba alizitaja meli zilizoshusha samaki kuwa ni Mv Tai HONG Namba 1 na Mv Tai HONG Namba 2 ambapo samaki watawekwa kwenye majokofu na kuuzwa soko la Feri. Alisema mbali na kushusha samaki, meli hizo zilikaguliwa huku zikitarajiwa kuchukua mabaharia wazawa wanne ambao watakuwa nao katika meli kama vigezo vya mahitaji ya lazima  ya Sheria navyodai.

 

Waziri Tizeba  aliitaka TPA kutoa kipaumbele kwa wenye meli hizo za uvuvi ili wasikae kwa muda mrefu na wazihudumie kwa haraka kwa kuwa zinabeba samaki ambao wanaharibika kwa haraka.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa meli hizo kwa nchi za Afrika, Simon Chen alipongeza jitihada za serikali ya Tanzania na Zanzibar kwa kuwahamasisha katika kupata leseni ya uvuvi wa samaki na akaahidi  kufanya  kazi kwa uaminifu mkubwa.

Alipokuwa Zanzibar Chen alisema kuwa bahari ya Tanzania inayo smaki wa kila namna na kinachofanyika ni kutengeneza ramani  na kukusanya takwimu za kusaidi kufanya kazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here