24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Tano Mwera:  Nilivutiwa na Bibi Titi nikaingia kwenye siasa

Na ASHA BANI



“MWAKA  2016 ni siku ambayo sitaisahau maishani mwangu kwa furaha niliyoipata baada ya kusikia kuwa nimeteuliwa na Rais John Magufulikuwa mkuu wa wilaya ya Busega.

“Nilijua moja kwa moja ndoto yangu imetimia, namshukuru Rais kwa kuniamini na kuniteua katika nafasi hii muhimu ya kuwahudumia Watanzania hasa wakazi wa Busega,” hivi ndivyo anavyoeleza Mkuu waWilaya Busega, Tano Mwera.

Alisema  nafasi hiyo ameipata wakati mwafaka, ambao alikuwa na kiu ya kufanya mambo mengi kwa ajili ya kuisaidia nchi yake hasa katika maendeleo.

Hata hivyo alieleza kutopata changamoto zozote pindi alipofika
kuripoti na kuanza kuchapa kazi kwani aliamini wanaBusega wanategemea

 maendeleo

“Lakini kwa kawaida huwezi kukubalika na kila mtu, wapo pia wanaoshangaa kuona Mkuu wa Wilaya mwanamke kwani walizoea kuona wakuu wa wilaya wanaume, lakini
sasa wameelewa tunaenda vizuri tu na tunachapa kazi za kuleta
maendeleo,’’alieleza Tano.

Malengo

Akizungumzia malengo ya Kiwilaya katika utendaji wake kwa mwaka 2017/2018  alisema lengo ni  kukuza elimu na tayari ameanza kuongeza vyumba vya madarasa kwa baadhi ya shule kwani tangu Sera ya Elimu Bure ianze uandikishaji  wa wanafunzi umeongezeka na wanaofaulu wameongezeka hivyo kuna  jukumu kubwa la kuongeza vyumba vya
madarasa na ikibidi shule mpya.

“Ni lazima kuongeza shule mpya maana huko tunakokwenda italazimika sasa kila kata kuwa na sekondari mbili badala ya moja na pia kuweka mikakati ya kukuza shughuli za uzalishaji katika sekta ya mifugo, kilimo, uvuvi na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili vijana  wapate ajira na kuondokana na  umaskini sambamba na kuanzisha mradi wa umwagiliaji mkubwa katika kata ya Mwamanyili,’’alisema Tano.

Alisema wilaya hiyo ina jumla ya  watu 203,597 kwa mujibu wa
sensa ya mwaka 2012 huku akazi wake wengi  wakitegemea kilimo na uvuvi .

Historia

Alianza shule ya Msingi mwaka 1981 na kumaliza mwaka 1987 katika shule ya Msingi Mkongo iliyopo Rufiji, Mkoa wa Pwani na kufaulu katika shule ya wasichana wenye vipaji maalumu ya Tabora Girls kuanzia mwaka 1988 mpaka 1991.

Alisema alifanya vyema pia na kufanikiwa kuchaguliwa kujiunga kwendakatika shule ya wasichana wenye vipaji maalumu ya wasichana ya Msalato Mwaka 1992/1994.

“Baada ya hapo nilifanya kozi fupi ya ‘front office Management’ na kuniwezesha kufanya kazi , White Sands Hotel kama telephone operator na baadaye British Council kama telephone operator/ secretary.

“ Mwaka 2001 nikajiunga Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kuchukua Advance Diploma ya Information Communication (ICT) kipindi ambacho pia nilikuwa nafanya kazi Wakala wa Barabara  (TANROADS) kama mtu wa
mapokezi na msaidizi wa rasilimali watu,’’alieleza Tano.

Alisema mwaka 2005 alimaliza IFM ambapo
mwaka 2007 alisomea Diploma ya Rasilimali watu katika chuo cha kifahari kiitwacho Varsity College kilichopo Mjini Cape Town.

“ Mwaka 2008 nikajiunga na Cape Peninsular University of Technology kusoma, BTECH Degree ya Business Administration na mwaka 2010 nikajiunga na University Of The Western Cape kuchukua Master Degree ya Public Administration.

“ Nikiwa Afrika Kusini nilifanya kazi katika sehemu mbali mbali ikiwamo 121 Group ni Call Centre Company, TAC – Treatmen Action Campaign NGO kubwa mjini hapo  inayopigania haki za matibabu kwa watu
wenye maradhi ya ugonjwa wa Ukimwi (HIV),’’alisema Tano.

Historia katika siasa

Kiilichomhamasishsa  kuingia katika siasa  ni kutokana na msukumo na kuguswa na matatizo ya jamii yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles