27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Tani 20 za korosho zakutwa kwenye ghala la mtu binafsi

Mwandishi Wetu

Tani 20 za korosho zimekamatwa kutoka ghala la mtu binafsi la Olam lililoko mkoani Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 17, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema korosho hizo zilikabidhiwa katika Chama cha Msingi cha Mnyawi kwa lengo la kuchanganywa kinyemela na zile zinazopelekwa kwenye maghala makuu.

“Jana (juzi) tulikamata tani 20 zilizokuwa zimepenyezwa katika vyama vya msingi, tusingependa lijirudie hivyo, wananchi wawe makini kuhakikisha korosho zinazoletwa katika vyama vya msingi ni zile za Watanzania ili korosho yetu peke yake iendelee kununuliwa na Serikali,” amesema Hasunga.

Amesema korosho zitakazokamatwa kutoka nje au kuingizwa kinyemela kwenye vyama vya msingi zitataifishwa na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Jumanne wiki hii tani nyingine tisa zilikamatwa katika eneo la Newala baada ya kuingizwa kinyemela toka nchini Msumbiji.

Aidha juzi pia yalikamatwa magunia 152 ya korosho katika Wilaya ya Nanyumbu yaliyoingizwa nchini kutoka Msumbiji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles