23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TANESCO YATOA SIKU NNE KWA WADAIWA SUGU

Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Umeme (TANESCO), limetoa siku nne wadaiwa sugu wa shirika hilo kulipa madeni yao.

Taarifa ilitolewa jana na Ofisi ya Uhusiano Tanesco, ilieleza kuwa iwapo wadaiwa watashindwa kulipa madeni yao watakatiwa huduma ya umeme.

“Tunautaarifu umma na wateja wetu wote kuwa tumetoa muda wa siku nne kuanzia Januari 12, 2018 (leo) hadi siku ya Jumatatu Januari 15, 2018 kwa wadaiwa sugu wawe wamelipa madeni yao.

“Baada ya muda huo kuisha shirika litasitisha huduma dhidi ya wateja watakaoshindwa kulipa madeni na litawachukulia za kisheria,” ilieleza taarifa hiyo.

Ilieleza zaidi kuwa ofisi za Tanesco zitakuwa wazi Jumamosi kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 9 mchana.

Hatua hiyo ni muendelezo wa agizo la Rais Dk. John Magufuli la Machi 5, mwaka jana alilolitoa akiwa Mtwara la kuwakatia umeme wadaiwa sugu wakati akizindua mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme wa 132kv mkoani Mtwara.

“TANESCO mmenifurahisha sana kwa kutekeleza vema ilani ya uchaguzi ya CCM, kwa kuhakikisha wanachi kote nchini wakiwemo wa vijijini wanapatiwa umeme,” alisema.

Alisema  anatambua changamoto zinazolikabili shirika hilo hususan madeni ya bili za umeme kwenye taasisi za serikali.

“Ninaagiza, wale wote wanaodaiwa bili za umeme na TANESCO walipe madeni yao haraka vinginevyo muwakatie umeme.

“Hata Ikulu kama inadaiwa we kata, najua pia kuna deni la shilingi bilioni 162 kule Zanzibar, nako kama hawatalipa kateni umeme. Tunataka TANESCO iharakishe kusambaza umeme kwa wananchi sasa wasipolipwa madeni watawezaje kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi?,” alihoji Rais Magufuli.

Alisema ofisi yake iko tayari kusaidia fedha pale itakapoonekana kuna mkwamo wa kifedha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.

Agizo hilo limeonekana kuwa na manufaa kwa TANESCO baada ya wadaiwa sugu wengi kujisalimisha kwa kuanza kulipia madeni yao ya umeme.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles