31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TANESCO KUDHIBITI WADAIWA SUGU

Na Upendo Mosha-MOSHI             |           


KATIKA kile kinachoelezwa kudhibiti madeni sugu ya umeme kwa idara na taasisi za Serikali, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Kilimanjaro, limeanza kazi ya kufunga mita za malipo ya awali (LUKU).

Taasisi ambazo zinafungiwa mita hizo ni zile zinazodaiwa madeni ya zaidi ya Sh bilioni tatu kwa vile  hatua hiyo itawasaidia kutumia huduma ya umeme kulingana na matumizi yao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Mahawa Mkaka, alisema shirika hilo limefikia uamuzi huo  kudhibiti kuongezeka  malimbikizo ya ankara za umeme kwa taasisi hizo.

Alisema shirika hilo limefanya mazungumzo na baadhi ya taasisi za serikali zinazodaiwa malimbikizo  makubwa  ya ankara za umeme na kukubaliana  kuwafungia mita za malipo ya awali waweze kuendelea kupata huduma ya umeme huku wakilipa madeni yao.

“Kuanzia sasa tumekubaliana shirika litawafungia mita za malipo ya awali mashirikia yote ya umma na madeni yao watayalipa kulingana na makubaliano yetu.

“Tunaamini suala hii itakuwa ndiyo njia pekee ya kumaliza madeni yao na kutoongezeka   madeni,” alisema Mkaka

Alitumia fursa hiyo kutangaza kwamba Tanesco limesitisha rasmi kukata umeme katika tasisi za serikali ambazo ni Jeshi la Polisi na Magereza kutokana na kuwapo  makubaliano maalumu.

“Jeshi la polisi na magereza hatutawakatia umeme ndani ya gereza wala kituo cha polisi ila katika nyumba za  polisi na askari magereza kila mtu atalazimika kujilipia bili zake za umeme kwa kutumia mita za luku tofauti na ilivyokuwa awali,” alisema Mkaka.

Alisema kazi hiyo itakwenda pamoja na operesheni ya kusimamisha umeme kwa baadhi ya taasisi za serikali ambazo zimeshindwa kufikia makubaliano na shirika hilo ya kufungiwa mita za luku na kulipa malimbikizo ya madeni yao.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles