Tamisemi waitikia agizo la JPM

0
950
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo, akionesha jengo jipya la ofisi za Tamisemi ambalo halijakamilika.

Na MAREGESI PAUL

-DODOMA

WAZIRI wa Tamisemi, Seleman Jafo, amehamia rasmi katika ofisi yake mpya ikiwa haijakamilika, iliyoko eneo la Mtumba katika mji mpya wa Serikali jijini hapa.

Kuhamia katika ofisi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli alilolitoa wiki iliyopita, wakati akizindua rasmi mji huo mpya.

Katika maelezo yake, Rais Magufuli alisema viongozi wa wizara hiyo pamoja na kwamba jengo lao halijakamilika, watatakiwa kuhamia hivyo hivyo kuanzia juzi Jumatatu.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli alisema wizara zote zitatakiwa kuhamia katika eneo hilo ili kila atakapokuwa akitaka kukutana na mawaziri, awafuate katika eneo hilo.

MTANZANIA lilifika eneo la ofisi hizo jana na kushuhudia ujenzi ukiendelea katika maeneo mbalimbali ya jengo hilo.

Akizungumza na MTANZANIA katika eneo hilo, Waziri Jafo alisema alilazimika kuhamia ofisini humo ili kuonesha ni kwa jinsi gani …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here