27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Tamasha la kumuenzi Nyerere kufanyika Oktoba 14

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



Kuelekea kumbukumbu ya 19 ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Kampuni ya Miranda Investment kwa kushirikiana na Chuo Cha Utalii Serengeti Media Center, wameandaa tamasha la kumuenzi litakayofanyika mkoani Mara, Oktoba 14, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Oktoba 4, mratibu wa tamasha hilo, Kulwa Karedia amesema tamasha hilo mahsusi la kumuenzi Baba wa Taifa litakuwa na michezo na mashindano mbalimbali yakiwamo mbio za baiskeli, mashindano ya riadha na mmkesha wa kuabudu.

“Tunatambua Mwalimu Nyerere alilifanyia taifa hili mambo ambayo hayawezi kufutika kamwe machoni mwa Watanzania, kutokana na msingi huo, tuliopo tunapaswa kumuenzi kwa kuyaendeleza yote mazuri aliyofanya kwa taifa hili hasa ukizingatia pia alikuwa mwanamichezo na alipenda michezo.

“Katika mashindano ya riadha itakayohusisha mbio za kilometa 10, mbio za kilometa tano kwa vijana wa miaka 13-18 na mbio za kilometa 2.5 hizi ni mbio za kujifurahisha,” Amesema Karedia

Karedia amesema tamasha hilo litafanyika katika kijiji cha Butiama alikozaliwa Mwalimu Nyerere pia litashirikisha wananchi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mara zikiwamo Tarime, Bunda, Musoma, Butiama, Serengeti na mikoa jirani.

“Mbio zote  zitaanzia Uwanja wa Mwenge Butiama kupitia Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kuelekea barabara ya Kiabakari ambayo Mwalimu nyerere aliitumia wakati wa kuunga mkono matembezi ya Azimio la Arusha mwaka1967,” amesema.

Mgeni rasmi wa mashindano hayo anatarajiwa kuwa Spika mstaafu, Pius Msekwa akiambatana na mkewe Anna Abdallah ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles