24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Taka hatarishi,vyuma chakavu sasa kubanwa na kanuni mpya

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM

SERIKALI imetangaza kanuni mpya za udhibiti na usimamizi wa taka hatarishi za mwaka 2019 baada ya kuifanyia marekebisho  ile ya  2009 iliyoonesha kuwa na mapungufu ili kuendana na kasi ya serikali ya Uchumi wa Kati na Viwanda.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Joseph Malongo alieleza sababu za kufanya marekebisho ya sheria hizo ni udhibiti wa biashara kwenye taka hatarishi na kufuata taratibu ikiwemo kukata vibali vinavyohitajika katika biashara hiyo.

Alisema kwa mwaka 2004 sheria hiyo kifungu namba  133 (1) na (93) cha sheria ya usimamizi wa mazingira kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya mazingira kutoa vibali  vya kuingiza, kusafirisha nje na ndani  ya nchi au kupitisha taka hatarishi nchini .

“Pia kanuni za mwaka 2009 zilitoa mamlaka hayo kwa Waziri na Mkurugenzi wa Mazingira lakini kwa mwaka 2019 marekebisho ya mamlaka ya kutoa vibali yamebaki kwa waziri mwenye dhamana ya mazingira tu akishauriwa na Mkurugenzi wa Mazingira,’’ alisema.

Pia alisema kanuni mpya ya mwaka 2019 zimeandaliwa kwa kuzingatia makundi ya aina za taka hatarishi kulingana na mkataba wa ‘Basel’ ambapo vyuma chakavu ni miongoni mwa taka zinazoweza kuwa hatarishi kwa kutegemea maeneo vinavyochukuliwa au vinakohifadhiwa au jinsi vinavyosafirishwa hasa pale vinapochanganywa kutoka maeneo tofauti.

Alisema katika kanuni ya mwaka 2009 hakukuwepo na masharti ya kuzingatiwa na mmiliki wa kibali kwamba suala hilo limezingatiwa katika kanuni mpya ya mwaka 2019.

“Uwepo wa masharti ya mmiliki wa kibali itarahisisha kufuatilia kwa mwenendo wa uzingatiaji wa masharti yaliyoainishwa katika kibali  cha usimamizi wa taka hatarishi pamoja na masuala ya hifadhi na usimamizi wa mazingira kwa ujumla wake,”.

Pia alisema kanuni za mwaka 2019 zimeeleza kuwa shehena yeyote ya taka hatarishi itakayoingizwa au kupitishwa nchini  bila kufuata masharti ya kanuni itachukuliwa kuwa ni usafirishaji haramu wa taka hatarishi na zinapaswa kurejeshwa katika nchi zilikotoka kwa gharama za msafirishaji au nchi husika zilizokotoka.

Injinia Malongo alisema pia kanuni 2019 zimeweka adhabu kali zaidi ukilinganisha na kanuni za mwaka 2009 kwa makosa ya kutokuwa na kibali cha kusimamia taka hatarishi nchini.

Alianisha adhabu hizo kuwa ni pamoja na faini ya shilingi milioni tano hadi bilioni 10 au kifungo kisichozidi miaka 12 au vyote kwa pamoja.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Mazingira (NEMC) Dk. Samwel Gwamaka alisema baraza halitamvumilia mtu yeyote atakayefanya biashara ya taka hatarishi pasipo kufuata utaratibu uliowekwa katika sheria hiyo mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles