TAIFA STARS KUKIPIGA CAPE VERDE OKTOBA 12

0
1011

Elizabeth Joachim, Dar es SalaamTimu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), itacheza mchezo wake wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon dhidi ya Cape Verde Oktoba 12,2018 na mchezo wa marudiano utachezwa Uwanja wa Taifa Oktoba 16,2018.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF),  Cliford  Ndimbo amesema kwa kushirikiana na Wadhamini wa Taifa Stars Bia ya Serengeti Premium Lager wanafanya utaratibu wa usafiri utakaoipeleka na kuirudisha timu hiyo kulingana na ratiba ya michezo hiyo ilivyokaa.

Amesema utaratibu wa Kambi/Kikosi Walimu watauzungumza ambapo utazingatia umuhimu wa mchezo,tarehe za kuondoka na za michezo yote miwili.

Ndimbo amesema pia unafanyika utaratibu wa kusafiri na mashabiki wa timu ya Taifa ambao watachangia gharama kidogo na ili kuweka hamasa ya kuelekea fainali hizo wameamua kuja na nukuzi (Hashtag) maalumu.

 

“Tumekuja na ‘Hashtag’ itakayotumika katika safari yetu ya kutupeleka Cameroon kwenye fainali hizo za mwakani ambayo ni #AfconCameroon2019ZamuYetu.

“Msimamo ulivyo mpaka sasa tunayo nafasi ya kwenda kwenye fainali hizo ambapo Uganda wanaongoza wakiwa na alama 4 ,Lesotho na Tanzania tuna alama 2 na Cape Verde wakiwa na alama 1,”amesema.

 

Aidha Ndimbo ametoa rai kwa vyombo vya habari na wadau mbalimbali kuungana na TFF kwakuwa ni sehemu muhimu na kuongeza hamasa katika safari hiyo ya kwenda Cameroon.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here