27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TAIFA STARS YANOGA

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

WACHEZAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, wanatarajia kuwasili leo kuungana na wenzao kujiandaa na mchezo dhidi ya Guinea ya Ikweta na Libya wa kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon2021).

Taifa Stars inatarajia kuanza kucheza dhidi ya Guinea ya Ikweta, Ijumaa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kabla ya kukutana na Libya Novemba 19, mwaka huu kuwania tiketi hiyo ya Afcon.

Timu hiyo iliingia kambini juzi usiku kuanza maandalizi ya michezo hiyo miwili ambapo walianza mazoezi jana jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mratibu wa timu hiyo, Danny Msangi, alisema wachezaji wanaocheza wote wanaocheza hapa nchini, wamesharipoti kambini huku anayecheza nje akiwa ni Hassan Kessy pekee.

“Wachezaji wanaocheza nje wanatarajia kuanza kuingia leo (jana) usiku, lakini kwa sasa ni Kessy peke yake ndiye ameshafika, lakini pia leo (jana) tutaendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa,” alisema.

Alisema wachezaji waliopo kambini wanaendelea vizuri na kila mmoja anaonekana kuwa na morali ya hali ya juu katika mazoezi yanayoendelea.

Wachezi walioitwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Etienne Ndayiragije ni makipa Juma Kaseja (KMC), Metacha Mnata (Yanga) na David Kisu (Gor Mahia Kenya).
Mabeki  ni Salum Kimenya (Tanzania Prisons), Hassan Kessy (Nkana  ya Zambia), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ Gadiel Michael, Erasto Nyoni(Simba) Bakari Nondo (Coastal Union), Kelvin Yondan (Yanga ) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Jonas Mkude, Hassan Dilunga Muzamiru Yassin (Simba), Abdulaziz Makame (Yanga), Simon Msuva (Difaa El Jadida ya Morocco), Eliuter Mpepo (Buildcon ya Zambia), Iddi Seleman, Abubakar Salum, Frank Domayo (Azam FC), Farid Mussa (Tenerife ya Hispania).

Washambuliaji ni Kelvin John (U-20), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania), Shaaban Iddi (Azam FC), Miraj Athumani (Simba ) na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk ya Ubelgiji).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles