31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TAEC yawakutanisha wataalamu nchi 21 kuboresha usalama, uhifadhi mionzi

Mwandishi Wetu, Arusha

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA), imefanya mkutano wa kimataifa kwa ajili ya kuboresha usalama katika kuhifadhi mabaki ya vyanzo vya mionzi.

Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Profesa Lazaro Busagala amesema mkutano huo wa siku tano umewakutanisha watalaamu 30 kutoka katika nchi 21 duniani unaoendelea jijini Arusha ambapo lengo kuu la mkutano huu ni kujadili kwa pamoja mkakati wa kuboresha usalama wakati wa kuhifadhi mabaki ya vyanzo vya mionzi ili kuepusha madhara ya vyanzo vya mionzi kwa binadamu na mazingira.

“Jukumu la kusimamia usalama wa vyanzo vya mionzi si la taifa moja, bali linahitaji ushirikiano wa nchi zote duniani ili kuhakisha kwamba vyanzo vyote vya mionzi vinakuwa katika mikono salama ili kuepusha madhara mbalimbali ikiwamo kutumika kwa vyanzo hivyo katika masuala ya ugaidi,” amesema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa IAEA, Dk. David Bennet amesema kwamba IAEA itaendelea kushirikiana na nchi wanachama ili kuhakikisha kuwa teknolojia ya nyuklia inatumika kwa matumizi salama.

Amesema vyanzo vya mionzi vinapomaliza muda wake wa matumizi vinahitaji kuhifadhiwa mahali salama na palipo na ulinzi maalumu jambo ambalo inasaidia kuepusha vyanzo hivyo kuzagaa na kusababisha madhara mbalimbali kwa binadamu na mazingira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles