33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TAEC yawafunda wafanyabiashara wa kahawa umuhimu wa kupima mionzi

Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Wafanyabiashara wa zao la kahawa mkoani Kilimanjaro, wamefadika na elimu ya umuhimu wa upimaji wa mionzi katika zao hilo iliyotolewa na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwenye soko la mnada uliofanyika wilayani Moshi mkoani humo.

Mnada huo uliofanyika leo Alhamisi Novemba 21, umewashirikisha wafanyabiashara mbalimbali wanaosafirisha kahawa ndani na nje ya nchi ambapo wamepata uelewa wa sababu za upimaji wa mionzi kwenye kahawa na utaratibu mzima wa upatikanaji wa  vibali vya kusafirisha zao hilo nje ya nchi bila kutumia mawakala .


Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Ufundi na Kinga ya Mionzi, Dennis Mwalongo akizungumza na wafanyabiashara wa kahawa kwenye mnada uliofanyika leo Novemba 21, wilayani Moshi mkoani kuhusiana na upimaji wa mionzi kwenye zao hilo.

Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia na Huduma za Ufundi wa TAEC, Dennis Mwalongo amewaambia wafanyabiashara hao kuwa lengo la elimu waliyoipata ni kuhakikisha Tanzania inaendelea kubakia katika soko la kahawa yenye ubora na isiyo na vimelea vya uchafuzi wa  mionzi.

“Tunawaelewesha hapa sababu za kupima mionzi kwenye kahawa kwani ni muhimu sisi kama taasisi tuna wajibu wa kuhakikisha madhara yatokanayo na mionzi hayatokei,” amesema Mwalongo.


Wafanyabiashara wa kahawa wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Ufundi na Kinga ya Mionzi wa TAEC, Dennis Mwalongo alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na upimaji wa mionzi kwenye zao hilo.

Sheria Na. 7 ya mwaka 2003 ya Nguvu za Atomiki Tanzani, imeipa mamlaka TAEC kudhibiti matumizi salama ya  mionzi nchini.

Kutokana na hali hiyo, amesema TAEC itaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara mbalimbali nchini juu ya kazi zake kwa lengo la kusaidia kutoa uelewa zaidi juu ya upimaji wa mionzi kwenye bidhaa mbali mbali zinazosafirishwa ndani na nje ya nchi.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles