23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TAEC mwenyeji warsha ya uzoefu kinga, udhibiti mionzi, nchi 23 zashiriki

Mwandishi Wetu, Arusha

Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA), inaendesha warsha inayohusisha wataalamu wa kitaifa wa kinga na udhibiti wa mionzi kutoka nchi 23 Afrika.

Washiriki hao ni nchi wanachama wa IAEA, ambapo lengo la warsha hiyo iliyoanza leo Jumatatu Novemba 4, ni kujadiliana uzoefu wa nchi za Afrika zilizopata kutekeleza viwango vya kinga na udhibiti wa mionzi  vilivyotolewa mwaka 2014 na Shirika la kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani na pia kujadili changamoto zilizowahi kujitokeza na kuzifanyia marekebisho.

Akifungua mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Profesa Lazaro Busagala amewataka watalaamu hao kujadiliana na kutoa mapendekezo sahihi yatakayosaidia kuwakinga wananchi na mazingira katika nchi zao dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha mionzi IAEA, Tony Colgan amesema washiriki wa mkutano huo wanapaswa kujadiliana na kupata mbinu zitakazowewazesha kuboresha ulinzi na usalama katika mionzi.

“IAEA inapenda kupata mrejesho wa uzoefu wa nchi hizo katika kutumia viwango hivyo vya kimataifa,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles