27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TAEC kuja na sheria mpya uchimbaji madini ya urani

Mwandishi Wetu, Arusha

Serikali kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Ulaya (EU) inaendesha warsha ya kuboresha shughuli za kisheria na uhakiki ili kuboresha uwezo uliopo katika kudhibiti madini ya urani.

Warsha hiyo kuanzia leo Jumanne Novemba 19 hadi 21, inafanyika katika Makao Makuu ya TAEC yaliyopo jijini Arusha ambapo lengo lake ni kujadili tathmini ya ripoti ya sheria ya udhibiti na mahitaji ya leseni ya uchimbaji wa madini ya urani.

Mkurugenzi Mkuu wa TAEC, Profesa Lazaro Busagala akifungua warsha hiyo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Wizara ya Madini, Dotto Biteko amesema majadiliano ya warsha yanalenga kuja na sheria mpya itakayoweza kutumika katika uchimbaji wa madini ya Urani pamoja na kumlinda mwananchi wa kawaida na madhara ya madini hayo.

“Kunahitajika udhibiti wa hali ya juu katika madini ya urani, hivyo sheria mpya itakapokamilika itaanza kutumika,” amesema.

Jumla ya washiriki 29 wanashiriki katika warsha hiyo ambapo kutoka TAEC na taasisi nyingine ambazo zinahusika katika masuala ya madini ya urani kama vile, Wizara ya Madini, Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Wizara ya Maji, Wizara ya Maliasili, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Tume ya Madini wanashiriki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles