23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tabaka la wasiojua kusoma, kuandika lawa historia

Na RAYMOND MINJA, IRINGA



SAMAKI mkunje angali mbichi, huu ni msemo wa wahenga, wenye maana ya kumlea mtoto katika maadili mema na kumfanya aishi na watu vizuri hapo baadae atakapofikia hatua ya kujitegemea.

Elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo, mtoto anapaswa kupewa elimu na malezi
mazuri ili kumjengea msingi bora wa maisha yake hapo baadae.
Mtoto ana haki ya kupata elimu nzuri kuanzia ngazi ya awali hadi elimu
ya juu.

Miaka kadhaa iliyopita, wanafunzi wengi wa shule za msingi walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya kuhitimu darasa la saba bila ya kujua kusoma na kuandika,
hii ilitokana na wanafunzi hao kutokuandaliwa vema tangu wakiwa
wadogo.

Kutokana na changamoto hiyo, Serakali iliamua kutafuta mwarubaini wa
jambo hilo na kuja na mbinu mbadala ya KKK ikiwa na maana ya Kuhesabu, Kusoma na Kundika, na sasa imeeanza kuonyesha mafaniko chanya mkoani
Iringa.

USAID Tusome Pamoja – ni mradi wa elimu wa miaka mitano unaofadhiliwa na
Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Watu wa Marekani (USAID).
Mradi huu unalenga kusaidia kuboresha stadi za ufundishaji na
kujifunza Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) katika shule za awali na
madarasa ya chini ya shule za msingi – kuanzia la kwanza hadi darasa la nne, katika mikoa ya Iringa, Morogoro, Mtwara na Ruvuma, pamoja na shule
zote za serikali zilizopo Zanzibar.

Pamoja  na kutoa mafunzo kwa walimu, vitabu kwa wanafunzi, malengo
zaidi ya mradi wa USAID Tusome Pamoja ni kuimarisha ushiriki wa wazazi
na jamii kwenye elimu kupitia kamati za shule, Ushirikiano wa Wazazi
na Waalimu ( UWAWA) na jamii yote kwa ujumla.

Miezi kadhaa iliyopita, USAID Tusome Pamoja walishirikiana na Serikali mkoani  Iringa kuendesha mafunzo ya  Mpango Jamii wa Uhamasishaji na Utekelezaji Elimu (MJUUE) wenye lengo la kuhamasisha jamii kubaini changamoto zilizopo kwenye  sekta ya elimu na zinazoathiri ubora wa elimu na ufaulu.

Mafunzo haya yalilenga kusaidia jamii kushiriki katika kuandaa
mipango ya elimu kwa ajili ya watoto wao hivyo, kuimarisha ushiriki wao katika kuboresha utoaji wa elimu kwa kuwa suala la maaendeleo ya shule linapaswa kufanywa na kila mwanajamii na si serekali pekee.

Kupitia mpango huo, USAID Tusome Pamoja ilitoa mafunzo ya siku tatu
kwa wawezeshaji jamii elimu 968 kutoka shule 481 za msingi za
serikali mkoani Iringa, ambao pamoja na mambo mengine wameweza kusaidia
kuongeza ulewa kwa washiriki.

Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe
wawili kutoka kila shule ya msingi wilayani Kilolo mkoni humo, kuhusu umuhimu wa jamii kushiriki shunguli za maendeleo ya shule, Ofisa
Mradi wa Tusome Pamoja, Wiston Ngowo, anasema jamii inapaswa
kutambuwa kwamba ina wajibu wa kusaidia maendeleo ya shule.

Ngowo anasema pamoja na kuwa mradi wa tusome pamoja ni kuhakikisha
wanafunzi wanajua Kusoma, Kuhesabu na Kuandika, lakini pia unawejengea
uwezo wazazi kujenga utamaduni wa kushiriki shughuli za
maendeleo ya shule zinazowazunguka na kuachana na dhana potofu ya kwamba
shule zinapaswa kuhudumiwa na Serekali pekee.

Ngowo anasema suala  la elimu ni la jamii nzima na si Serekali pekee, na kwamba mabadiliko makubwa ya elimu yataletwa na wananchi wa sehemu husika – hayawezi kushuka kama baraka kutoka mbinguni.

Anasema mradi wa Tusome Pamoja uliobuniwa na Serekali na
kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Watu wa Marekani
(USAID), umesaidia kwa kiasi kikubwa kubadili mawazo hasi waliyokuwa
nayo wanananch juu ya kushiriki shunguli za maendeleo ya shule ikiwamo kujenga miundombinu ya shule kama vyoo bora kwa ajili ya watoto wao.

“Unajua apo awali wazazi wengi walikuwa ni wagumu kushiriki shunguli za maendeleo ya shule wakidhani kila kitu
kinatakiwa kufanywa na serekali, lakini baada ya mafunzo tuliyoyatoa
wamaebadilika na matokeo chanya yameanza kuonekana kwa kila shule,” anasema.

Ngowo anasema mradi huo umefanikiwa kutoa elimu kwa walimu na maafisa
elimu ikiwamo kutoa mafunzo ya KKK ili kumsaidia mtoto wa darasa la
kwanza na la pili kujua kusoma na kuandika.

Anasema mara baada ya kutoa mafunzo hayo kwa walimu, wameona
mafanikio makubwa ambayo bado hawajayaweka kwenye asilimia kwa kuwa
zoezi bado linaendelea, lakini kwa mtazamo wa nje mafanikio
yanaonekana.

“Tumetoa mafunzo kwa walimu na kuwapa mbinu za kufundishia, unajua
walimu wengi walikuwa wakifundisha kwa mazoea, lakini baada ya mafunzo hata wao wanakiri mafanikio waliyopata na sasa wanafurahia kazi yao ya ualimu,” anasema.

Kwa upande wake Mratibu wa maradi huo kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa
Iringa, Keneth Komba, anasema mradi huo umekuwa msaada mkubwa kwa
serekali kwani umewatua mzigo mzito uliokuwa ukiwaelemea wa kuhudumia
mambo mengi katika shule za serakali.

Komba anasema mradi huo uliobuniwa na serekali umeleta
matokea chanya ikiwamo wazazi na walezi kuweza kushiriki shughuli
za kimaendeleo katika shule zinazowazunguka na wanafunzi
kunza kufanya vema katika KKK.

“Huu mradi ni muhimu kwa mkoa wetu wa Iringa, utazifikia shule za
msingi 481 zilizoko mkoani hapa ili kuweza kutoa mafunzo
juu ya wanafunzi kujua kusoma na kuandika pia ushiriki wa wazazi
katika maendeleo ya shule,” anasema.

Komba anasema tangu mradi huo uanze, umeongeza uelewa kwa walimu na hivyo kufundisha kisasa si kama ilivyokuwa awali.
Mmoja ya washiriki katika semina hiyo, Akram Lungali, kutoka
Kijiji cha Ihinganatwa wilayani Mufindi, anasema mradi wa
Tusome Pamoja umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwabadili mawazo wazazi
wengi waliokuwa hawatekelezi majukumu yao ipasavyo, na sasa matunda
yameanza kuonekana.

Lungali anasema mara baada ya kupewa mafunzo hayo, wamefanikiwa
kuanza ujenzi wa madarasa matutu kwa ajili ya wanafunzi kujisomea na
baada ya kuonyesha jitihada hizo, walifanikiwa kupata msaada wa mabati
60 na mifuko ya saruji 60 kutoka kwa Mbunge wao Mendrad Kigola.

Akizungumzia matokeo chanya ya mradi wa Tusome Pamoja KKK, anasema yeye
ni mmoja wa wazazi waliona mabadiliko makubwa kwa watoto wao baada ya
mradio huo kutoa mafunzo kwa walimu wa awali, kwa kuwa walimu sasa wanafundisha kwa ufanisi zaidi.

Anasema hapo awali kulikuwa na watoto ambao wanahitimu shule ya msingi bila kujua kusoma na kuandika lakini sasa mambo yamebadilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles