30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi za dini hazijafanyiwa tathimini ya tetemeko -Askofu

1

Na EDITHA KARLO, KAGERA

VIONGOZI wa dini mkoani Kagera wameishauri Serikali kushirikisha wananchi katika kutathimini madhara yaliyotokana na tetemeko la ardhi mkoani humo.

Walisema mpaka sasa baadhi ya maeneo kama yale yanayomilikiwa na taasisi za dini hayajafikiwa na kufanyiwa tathimini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini, alisema wanapaswa kufanya tathimni mbili.

“Tathimini ya kwanza ni ile ya haraka na kuwatafutia watu maeneo ya kulala kama vile mahema, chakula na dawa pili kufanya tathimini ya kuhusu majengo na kutafuta njia ya kupata vifaa vya ujenzi ili kujenga majengo au nyumba imara.

“Sisi kama viongozi wa dini hatujaona watu wanakuja kufanya tathimini katika makanisa yetu yaliyoathirika,nyumba za mapadre zimeanguka,wakitaka tathimini ifanikiwe na kutoa majibu ya uhakika watushirikishe sisi jamii, watu wanataabika mvua zitaanza hivi karibuni, watu wanaendelea kulala nje,wengine hawafikiwi na wakiendelea hivyo bila kushirikisha jamii  hari hiyo itachukua muda mrefu huku watu wakiendelea kuathirika”alisema Askofu Kilaini.

“Sisi tumepata hasara kubwa kutokana na hili janga, kanisa letu la Ihungo limeanguka, nyumba ya kihistoria iliyojengwa mwaka 1940 iliyokuwa ikitumiwa na mapadre katika kanisa hilo la Ihungo imeanguka.

“Kwa hiyo lazima tujenge upya, kanisa la kihistoria ambalo ni kanisa la kwanza mkoani Kagera lililojengwa mwaka 1892 na ndio chimbuko la dini yetu hapa Bukoba pia limeharibika kabisa tunahitaji msaada wa haraka kulikarabati pia,”alisema Askofu Kilaini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles