23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

T-PAIN AKAMATWA NA POLISI



ATLANTA, MAREKANI

STAA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Faheem Rashad Najm maarufu kwa jina la T-Pain, amekamatwa na polisi kwenye uwanja wa ndege wa Atlanta huku akiwa na bunduki kwenye begi.

Inadaiwa kuwa, bunduki hiyo aina ya Smith & Wesson Bodyguard 380, ilionekana wakati wa upekuzi huku msanii huyo akiwa anaelekea jijini Texas kwa ajili ya tamasha la Back 9ine Fest 2018.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, msanii huyo mwenye umri wa miaka 32, alichukuliwa na polisi huku akiwa amenyang’anywa silaha na kupelekwa kituoni kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Hata hivyo, haijulikani kama msanii huyo aliachiwa huru au aliwekwa ndani, lakini huku tamasha hilo likiendelea msanii huyo alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuposti picha ya boksi likiwa limefungwa kufuli, posti hiyo imewaacha na maswali mengi mashabiki huku wakiamini kuwa msanii huyo amewekwa ndani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles