24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Sura mbili za rapa Cardi B zinavyomuhukumu

NEW YORK,MAREKANI

AKIWA na miaka 19, rapa nyota ulimwenguni, Belcalis Almanzar maarufu kama Cardi B, alijiingiza kwenye vikundi vya warembo wanaotumia miili yao kujipatia fedha, ikiwa ni muda mfupi baada ya kufukuzwa kazi ya kuuza bidhaa kwenye moja ya duka kubwa huko Lower Manhattan, New York, Marekani.

Cardi B (26), ambaye  kwa sasa ni msanii anayeshikilia tuzo ya Grammy katika kipengele cha Albamu Bora ya Rap 2019 kupitia albamu ya Invasion of Privacy, ndani ya sura ya kwanza ya maisha ya uchojoaji (changudoa), alilazimika kufanya kazi hiyo ili aweze kuukimbia umasikini, kukimu mahitaji yake na ya familia.

Rapa huyo anayetamba na wimbo, Please Me aliomshirikisha Bruno Mars, alianza kujizolea umaarufu mtandaoni kupitia video chafu za kutingisha makalio mwaka 2013, kabla ya kuonekana kwenye kipindi cha runinga VH1 kinachoitwa Six Of Love & Hip hop, kilichomwingiza rasmi kwenye tasnia ya burudani hususani muziki wa rap.

SURA YA KWANZA INAVYOMUHUKUMU

Kama nilivyotanabaisha hapo juu kuwa Cardi B ana maisha yenye sura mbili ambazo zote hizo hivi karibuni zimeonekana kumpa hukumu. Sura ya kwanza ni ile ya maisha ya uchangudoa na sura ya pili ni Cardi B mpya ambaye hapendi wasichana wengine waishi maisha aliyowahi kuishi yeye.

Hivi karibuni Cardi B, aliweka wazi maisha ya ufuska aliyokuwa akiishi miaka mitatu iliyopita jambo ambalo limekuwa gumzo katika mitandao mbalimbali hasa Twitter kwa kile alichosema alikuwa anatumia dawa za kulevya kuwalewesha wanamume kisha kuwaibia fedha zao.

Cardi B, anasema katika sura ya kwanza ya maisha yake ya ‘u-stripper’, alikuwa anawakubalia wanamume kufanya nao ngono na wakishaingia chumbani anawarubuni na kuwawekea dawa za kulevya kwenye vinywaji na jamaa wakipoteza fahamu, anazama mfukoni, anaiba fedha na kutokomea.

Mrembo huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike anayeitwa Kulture aliyezaa na rapa wa kundi la Migos, Ofset, alibainisha kuwa anajutia kuishi maisha hayo na hajawahi kujivunia hata siku moja.

Wanamume mbalimbali waliowahi kuumizwa na warembo kwa mtindo wa kuwekewa dawa za kulevya, wamepaza sauti zao wakitaka mamlaka za usalama nchini Marekani zimchukulie hatua za kisheria Cardi B hasa ukizingatia haki za binadamu zimekuwa zikiangalia upande mmoja tu wa wanawake na kuwasahau wanamume ambao wanaumizwa na vitendo hivyo.

SURA YAKE YA PILI INAVYOMTETEA

Maisha ya sasa ya Cardi B, yanawavutia wasichana wengi wapambanaji. Wanatamani kujifunza mema kutoka kwake kutokana na vile anavyotumia muda mwingi kuchapa kazi.

Kwa hapa Bongo jaribu kusikiliza nyimbo za kina Gigy Money (Kiki ni Gigy), Queen Darleen (Muhogo) utagundua marapa wengi wa kike wanachukua vionjo, mikogo na miondoko ya Cardi B.

Sura ya pili ya maisha ya Cardi B ndani ya sanaa, tunaona amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kugusa maisha ya watu mbalimbali hasa wahitaji, kwani mrembo huyo tajiri amekuwa akitoa misaada kwa wasichana wenzake wanaoishi maisha magumu, wazee, wagonjwa, yatima nk.

Ndiyo maana kumekuwa na mvutano mkali mtandaoni baina ya watu wanaotaka Cardi B ashtakiwe kutokana na maisha ya sura yake ya kwanza ya uchangudoa na wengine wakitaka atumike kama funzo kutokana na maisha yake ya sasa.

CARDI B, J LO KUJA NA FILAMU

Tayari mrembo huyo, ameingia mzigoni kucheza filamu yake mpya inayoitwa Hustlers, iliyobeba maudhui ya maisha ya warembo wanaojiuza, lengo likiwa ni kutoa elimu kwa jamii hasa wasichana kuhusu kuepuka maisha hayo na jinsi serikali inavyoweza kuwaboreshea mazingira ya kazi.

Ndani ya filamu hiyo itakayochezwa katika mitaa ya New York, Cardi B, ataigiza akishirikiana na mwanamuziki Jennifer Lopez ‘J Lo’, waigizaji Lili Reinhart, Keke Palmer, Julia Stiles na Constance Wu huku mwongozaji akiwa ni Lorene Scafaria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles