31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

SUMATRA KAGERA KUFANYA SENSA VYOMBO VYA USAFIRI 

 

Na Renatha Kipaka

SUMATRA mkoani Kagera wanatarajia kufanya sensa ya vyombo vinavyofanya safari katika visiwa mkoani humo ili kuvitambua vyenye usajili na ambavyo havijasajiliwa.

Kauli hiyo ilitolewa na Ofisa Mfawidhi Sumatra Kagera, Patrick Mipawa   alipozungumza   na waandishi wa habari mjini Bukoba.

Alisema   kutokana na Mkoa wa Kagera kuwa na visiwa vingi na vyombo vingi vinavyosafirisha watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine,  sensa ni muhimu  kubaini uhalali wa vyombo hivyo.

Alisema   hatua hiyo itakuwa ni pamoja na kuwabaini kwa mujibu wa sheria waendeshaji wa vifaa hivyo kama wamepitia   mafunzo au wanaendesha vyombo hivyo kwa uzoefu.

Ofisa huyo alisema  atika vyombo hivyo kuna vilivyopo kwa mujibu wa sheria ambavyo ni vya uvuvi au kubebea mizigo.

Mipawa  alisema vyombo vinavyosafirisha abiria na mizigo pamoja na uvuvi ni zaidi ya 4,000 wakati vyombo vinavyosafirisha abiria ni 159 na vya mizigo ni 53 wakati vya uvuvi ni 3853.

“Mimi binafsi naona mkoa huu una vyombo vingi vya mbao tofauti na sehemu nyingine na   uimara wake si mzuri.

“Kwa jinsi hiyo vinatakiwa kufanyiwa marekebisho mara kwa mara ili viwe imara na kuepuka ajali,” alisema.

Medadi Yohana anayefanya kazi   katika boti ya MV Mwanzo kutoka Bukoba kwenda   kisiwa cha Kerebe, alisema  changamoto inayowakali ni ukosefu wa taarifa sahihi za hali ya hewa.

“Kwa upande wangu sina shaka na Sumatra tunashirikiana nao vizuri.

“Shida inakuja  tunapokosa taarifa zilizo sahihi na kujikuta tukikumbana na dhoruba kwenye maji wakati tuko safarini,” alisema Yohana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles