31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Suluhu ya Ukawa, CCM yakwama

Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi

Patricia Kimelemeta na Grace Shitundu

KIKAO kati ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kimeshindwa kupata muafaka baada ya pande hizo mbili kuendelea kuvutana hadi jana jioni.

Kikao hicho cha siri kilichoanza jana saa nne asubuhi katika Hoteli ya Sea cliff iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam, kiliongozwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Fransis Mutungi.

Jaji Mutungi aliingilia kati suala hilo, baada ya kuona muafaka wa Ukawa kurudi bungeni umekwama kutokana na madai ya wajumbe wa CCM wanajadili mambo yasiyokuwamo ndani ya rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Jaji Joseph Warioba.

Madai mengine ya Ukawa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kutumia madaraka yake vibaya ikiwa ni pamoja na kupindisha kanuni za Bunge hilo.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Mutungi alilazimika kuwaita viongozi wa CCM na Ukawa ili waweze kuwapatanisha ikiwa ni pamoja na kuwataka Ukawa warudi bungeni katika kikao kijacho ambacho kinatarajiwa kuanza Agosti 5, mwaka huu.

Ukawa unaundwa na vyama vitatu vya Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha NCCR-Mageuzi.

Akizungumza na MTANZANIA kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu, alisema mpaka  jana jioni hakuna muafaka katika kikao hicho kutokana na kuendelea kuvutana.

“Nimetoka kwenye kikao lakini hakuna muafaka, hii inatokana na pande mbili kuendelea kuvutana, kwa hiyo nimewaacha waendelee kujadili suala hilo,” alisema Lissu.

Alisema msajili ndiye aliyeitisha kikao hicho ikiwa ni pamoja na kutafuta muafaka wa suala hilo, lakini kwa dalili zinazoonekana hakuna muafaka hapo.

Hivi karibuni, Ukawa walidai kuwa hawawezi kurudi tena kwenye Bunge hilo mpaka wajumbe hao wa CCM watakapokubali kujadili rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Jaji Warioba.

Kumekuwa na juhudi mbalimbali za kutafuta muafaka kuhusu suala hilo ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini, taasisi za kiraia na wadau mbalimbali ambao kwa pamoja wamekuwa wakiwasihi Ukawa warudi bungeni ili kujadili rasimu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

  1. Biblia inasema “wanga na giza” haziwezi kukaa pamoja. Ukweli na uwongo lazima vijitenge, upendo na chuki havuwezi kukaa amoja, shetani na Mungu hawawezi kuwa sehemu moja. JAMANI, UKWERLI TUNAUJUA NANI KAHARIBU MCHAKATO WA KATIBA, KWANINI walioharibu mchakato wa katiba ambao ni CCM wasikubali ili tusonge mbele. Nawapongeza Ukawa kwa msimamo wa kutetea maoni ya wananchi chini ya Tume ya jaji Msitaafu Warioba Sinde. Mungu atawaonyesha wabaya wa katiba moya muda si mrefu Amina.

  2. Jamani jilazimisheni kuliona tatizo siyo kulifumbia macho kiasi hivho.Hivi wewe msajili wa vyama unaacha kuwashawishi CCM kujadili kilicholetwa ma tume meza ili mambo yaende mbele unawang’ang’aniza Uwaka kurudi bungeni ilihali unajua hawako tayari kuwasiliti watanzania wenzao katika jambo ya msingi kama.Acheni kitufanya watanzania hatuna akili.Mimi tatizo nalijua na dawa ya tatizo ni CCM kuingia bungeni nakujadili mawazo ya watanzania wenyewe akili timamu kama yalivyowasilisha bungeni na tume ya jaji mwenye hekima ya kutosha na mwenye kuijua Tanzania vizuri Joseph Sinde Warioba na si vinginevyo huo ndiyo muarubani wa kupatikana kwa Katiba yenye kumjali mbongo bila kujali kipato cha mbongo hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles