Sugu amuita Mbunge wa Serengeti poyoyo

0
2313

Mwandishi Wetu, Dodoma

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (CHADEMA) amemuita Mbunge wa Serengeti Marwa Ryoba (CCM) kwamba ni poyoyo.

 Sugu ametoa kauli hiyo leo Aprili 11,  bungeni jijini Dodoma alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Tamisemi, Utumishi na Utawala bora kwa mwaka wa fedha 2019/20, ametumia neno hilo baada ya mbunge huyo wa CCM kuomba mwongozo na kumshangaa mbunge huyo wa mbeya mjini kusema Tanzania hakuna Tume huru ya uchaguzi.

Hata hivyo baada ya Sugu kutumia neno hilo wabunge walilipuka kwa vicheko na kumfanya Mnadhimu Mkuu wa serikali bungeni  Jenista Mhagama asimame huku akicheka na kumtaka afute neno poyoyo kwa sababu siyo neno la kibunge.

Aidha kutokana na hali hiyo Mwenyekiti wa Bunge,Najma Giga alimtake afute neno hilo kwa kuwa hata yeye halijui maana yake, kutokana na maagizo hayo Sugu aliamua kufuta neno hilo na kuahidi kulitumia nje ya Bunge.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here