30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

 Soudy Brown, Shafii Dauda wafikishwa mahakamani

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam
Watangazaji wa Kituo cha Clouds, Soud Kadio maarufu Soudy Brown wa kipindi cha Shilawadu, na Shafii Dauda wa Sports Extra, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kutumia maudhui mtandaoni bila kuwa na kibali.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani leo Jumatatu Septemba 24, na kusomewa mashtaka yao ambapo Brown amesomewa na Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nguka akishirikiana na wakili Estazia Wilson na Dauda akisomewa Wakili wa Serikali Mkuu Tumaini Kweka akishirikiana na mawakili Mutalemwa Kishenyi na Mwanaamina Kombakono ambapo wamedai kati ya Juni na Septemba washtakiwa walitumia maudhui mtandaoni bila kuwa na kibali.

Mshtakiwa Brown anadaiwa kuwa kati ya Juni 11 na Septemba mwaka huu kwa kutumia online Tv inayojulikana kwa jina la Shilawadu Tv huku Dauda akidaiwa kati ya Juni 14 hadi Septemba mwaka huu kwa kutumia online Tv inayojulikana kwa jina la Shafii Dauda kinyume cha sheria walitoa na maudhui katika mitandao hiyo bila kibali kutoka mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Mshtakiwa Brown amesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustino Rwizile na Dauda amesomewa mashataka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina.
Mawakili wa utetezi Peter Kibatala wa Brown Jebra Kambole wa Dauda waliomba wateja wao wapewe dhamana kwa sababu mashtaka yanadhaminika.

Hakimu Rwizile alikubali kumpa dhamana mshtakiwa Brown kwa masharti ya kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni mbili na mshtakiwa mwenyewe asaini dhamana ya kiasi hicho cha fedha na Hakimu Mhina alikubali kumpa dhamana Dauda, amemtaka  kuwa na wadhamini wawili  wawe na vitambulisho vya kuwatambulisha na barua ambazo zinatambulika.

Washtakiwa wamefanikiwa kukamilisha masharti ya dhamana na kuachiwa huru , kesi ya Brown imeahirishwa hadi Oktoba 18 huku ya Dauda ikiahirishwa hadi Oktoba 8, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles