24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

SOPHIA SIMBA AREJEA KUNDINI

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya cha Chama Cha Mapinduzi (NEC), kwa kauli moja kimemrudishia uanachama wa chama hicho, aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Simba baada ya kuomba radhi.

Sophia Simba alivuliwa uanachama wa chama hicho Machi mwaka huu, pamoja aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida huku Emmanuel Nchimbi na Adam Kimbisa wakipewa onyo kali kwa madai ya kukisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Katika kikao hicho kilichoketi jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amesema, alipokea barua kadhaa kutoka kwa Sophia ambapo moja aliisoma mbele ya kikao hicho, akiomba kusamehewa na kurejea CCM ambapo aliomba ridhaa ya wajumbe kumpokea endapo wameridhia ambapo kwa kauli moja walikubali.

“Katika wote tuliowafukuza na tuliowapa adhabu huyu ndiye ameandika barua ya kuomba radhi na wengine wawili wao waliandika tu wanakubaliana na maamuzi yaliyotolewa wengine walikaa kimya tu mpaka leo hawajasema chochote. Sasa niliguswa na huyu ambaye aliomba radhi mara nyingi,” amesema Rais Magufuli.

Katika sehemu ya barua yake hiyo, Sophia amesema: “Nakubali adhabu niliyopewa ambayo ilitolewa na vikao halali, aidha naandika barua hii kuomba mnisamehe kwa sababu maisha yangu yote kuanzia kwa wazazi wangu nimekuwa ndani ya TANU na CCM na kila kiilichofanikiwa hapa duniani basi nimekipata kwa sababu ya CCM chama nikipendacho na kuikithamini.

“Naomba radhi tena kwani  mzigo huu ni mzito sana na sijui jinsi ya kuubeba na ni adhabu yangu ya kwanza na ndiyo adhabu kubwa na ya mwisho naomba mnihurumie. Naamini katika chama kuzaliwa upya.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles