25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

SOMO LA NIDHAMU LIMEWAINGIA MASHABIKI SIMBA, YANGA

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

MIAKA ya nyuma tulikuwa tukishuhudia mechi kati ya Simba na Yanga zikimalizika kwa vurugu, zikiongoza kwa utovu wa nidhamu kutoka kwa mashabiki.

Taratibu somo la kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake kwa kulinda heshima yake limeanza kuwaingia mashabiki wa timu hizi mbili.

Mchezo uliofanyika juzi katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, uliweza kumalizika kwa amani huku matokeo yakiwa ni 1-1.

Hongera mashabiki kukubaliana na matokeo, maana imezoeleka na kushuhudiwa waamuzi, wachezaji na makocha  wakifanyiwa fujo, huku wengine wakiamua kupigana wenyewe kwa wenyewe.

Pongezi ziwaendee mashabiki waliojitokeza uwanjani kushuhudia timu hizi mbili, ambazo kila zikutanapo hukusanya hisia za wadau wengi wa soka.

Mchezo huo ulishuhudiwa ukianza na kufikia tamati kwa nidhamu ya hali juu, vurugu za ajabu ajabu ambazo zimekuwa zikijitokeza miaka ya nyuma hazikuweza kuwepo.

Hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa, hivyo ni vema mashabiki wa klabu za Simba na Yanga wakajitambua na kuendelea kuwa wavumilivu, wanyenyekevu pindi timu zao zinapokutana.

Nidhamu ya  namna hii inaweza kurejesha uaminifu kwa Serikali yetu inayosimamia Uwanja wa Taifa,  ambao kwa asilimia kubwa mechi za Simba na Yanga zimechangia uharibifu mkubwa ndani ya uwanja huo.

Kitendo cha timu hizo kufungiwa kutumia uwanja huo kwa makosa mbalimbali ni aibu, kwani inaonyesha jinsi gani mashabiki wanashindwa kujitambua.

Mpira ni moja ya burudani tosha, unapogeuzwa kuwa ugomvi au malumbano unapoteza thamani na kupelekea burudani yote kuonekana ya ovyo.

Umefika wakati mashabiki kujitambua na kuacha dhana ya kusababisha vurugu viwanjani, kwani kwa kufanya hivyo soka letu haliwezi kupiga hatua bali tutaendelea kubaki nyuma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles