24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Solskjaer atengewa pauni milioni 250 za usajili

LONDON, ENGLAND

KLABU ya Manchester United, imetenga bajeti ya pauni milioni 250 sawa na Sh bilioni 731 za Tanzania kwa ajili ya kocha wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer, kufanya usajili wa wachezaji wapya majira ya joto.

Manchester United imemaliza msimu ikiwa nafasi ya sita ukiwa ni msimu mbaya kuwahi kutokea katika historia ya klabu hiyo baada ya kufungwa michezo nane kati ya 12 ya kumalizia msimu.

Kocha Solskjaer, atalazimika kukitengeneza upya kikosi chake kwa kufanya usajili katika majira ya joto.

Gazeti la The Times, linaeleza kuwa kocha huyo tayari ametengewa pauni milioni 250 kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo,  Ed Woodward, ambaye amedhamiria kuirejesha timu hiyo kwenye makali yake msimu ujao. 

Klabu hiyo inataka kumsajili beki wa kulia wa Crystal Palace, Aaron Wan-Bissaka na beki wa West Ham, Declan Rice, huku kiungo wa  Sporting, Bruno Fernandes na Atletico Madrid, Saul Niguez, pia wakiwa miongoni mwa wachezaji wanaotakiwa na klabu hiyo majira ya joto.

Manchester United pia ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Swansea City kuhusu usajili wa kiungo wao, Daniel James (21) na klabu ya Lille wakiitaka wamwachie mshambuliaji wao, Nicolas Pepe, ambaye ameweka kambani mabao 20 na kutoa pasi 11 za mabao msimu huu.

Tayari beki wa kati wa Ajax, Matthijs De Light, ameweka wazi matarajio yake ya kucheza Manchester United msimu ujao licha ya saini yake kusakwa kwa muda mrefu na klabu ya Barcelona.

Wakati huo huo, kiungo wa Newcastle United, Sean Longstaff, ameunganishwa kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa na klabu ya Manchester United kurithi mikoba ya Ander Herrera, ambaye anatarajiwa kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles