28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Solskjaer amkingia kifua Paul Pogba

MANCHESTER, ENGLAND

BAADA ya kiungo wa Manchester United, Paul Pogba kukosa mkwaju wa penalti juzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Wolves, kocha wa timu hiyo Ole Gunnar Solskjær amemkingia kifua Pogba na kudai mtu yeyote anaweza kukosa.

Mchezo huo ambao Wolves walikuwa nyumbani, ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, huku Manchester United wakiwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao Anthony Martial kabla ya Ruben Neves kusawazisha kipindi cha pili.

Hata hivyo Manchester United ilifanikiwa kupata mkwaju wa penalti ambao ulikuwa unagombania na wachezaji wawili kutaka kupiga, Pogba na Marcus Rashford, lakini Pogba alipiga na mlinda mlango wa Wolves, Rui Patricio aliucheza.

Kitendo hicho cha Pogba kuchukua jukumu la kupiga penalti na kukosa kimewachukiza mashabiki wengi, lakini kocha wa timu hiyo ameonekana kumtetea mchezaji huyo.

“Tulipata nafasi ya penalti ambayo ingeweza kutufanya tuwe na pointi tatu kama tungefanikiwa kushinda, lakini mlinda mlango alikuwa makini na kufanikiwa kuicheza.

“Wote wawili Rashford na Pogba ndio ambao wanahusika kwenye kupiga penalti, hivyo ni juu yao wenyewe kuamua nani apige kati yao na hakuna ambaye anawapangia.

“Kuna wakati wachezaji wanajiamini kuwa wanaweza kufunga bao, Pogba amekuwa akifunga mabao mengi kwetu, lakini kipa wa Wolves alikua kwenye ubora wake na kufanikiwa kuicheza, mtu yeyote anaweza kukosa penalti,” alisema Solskjaer.

Kocha huyo aliongeza kwa kusema, hata kama Pogba alikosa mkwaju huo wa penalti bado yeye na mwenzake Rashford watakuwa na jukumu hilo la kupiga labda wao wenyewe waamue kuacha.

“Nimekuwa nikiwapenda wachezaji ambao wanajiamini kwenye suala la kupiga penalti hivyo Pogba na Rashford ni miongoni mwao na ndio maana nimewapa nafasi hiyo, lakini wao wanaweza kumpa mtu mwingine kama watajisikia hawawezi kupiga,” aliongeza

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles