24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Smart Lab Kuunganisha Wavumbuzi na Viongozi wa makampuni

Mwandishi wetu

Wakala wa digitali na Teknolojia nchini, Smart Lab, wameunda jukwaa linalolenga kuwaunganisha wabunifu na viongozi wa juu wa mashirika ili kubadilishana uzoefu wao na safari yao ya kitaalam katika kuhamasisha ukuaji miongoni mwa wazalishaji nchini.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Smart Codes, Edwin Bruno alipokuwa akizungumza katika Makao makuu ya kampuni hiyo Mikocheni jijini Dar es salaam ambapo amesema wanaamini katika kuunda na kuhamasisha wabunifu, kampuni changa, wajasiriamali, mashirika na vyama vingine vya uwajibikaji kujifunza kutoka kwa kila mmoja juu ya jinsi ya kufanya kazi katika mfumo unaobadilika wa kubadilisha ekolojia.

“Tuko kwenye njia ya kufunga pengo kati ya taasisi za elimu na kampuni changa ambayo itapelekea kuunda bidhaa zenye ubora, suluhisho na huduma za juu ambazo zitatatua matatizo ya msingi katika jamii, Kwa kuhusisha uwezo wa wanafunzi, wazalishaji na kampuni changa na kuwapa vifaa vya kuwasaidia kupitia programu tofauti kama “Corporate Unwind” wataweza kupata uhalisia uliopo katika jamii ya mashirika  ambayo itawapelekea kutoa matokeo mazuri kwa pande zote mbili,” amesema.

“Kama moja ya kitovu cha uvumbuzi kinachojihusisha na kampuni changa kila siku, tuliweza kugundua uwepo wa pengo hili hivyo tukawaalika wafanyabiashara waliofaulu na wenye uzoefu mkubwa katika sekta tofauti kuungana nasi kwa majadiliano ya kujumuisha na kubadilishana mawazo ambayo yatakuwa na faida kwa kulenga kile kinachohitajika kukuza mfumo wa ekolojia na mwisho wa siku kuja na suluhisho la soko linalofaa,” amesema.

Aidha amesema kuwa hii ni hatua ya kwanza katika madhumuni makubwa ya kujenga jamii ya wajasiriamali, wawekezaji na wafuasi wa ikolojia kwa kushirikiana na  sekta ya biashara na ubunifu, lengo likiwa ni kuunda fursa kwa wavumbuzi, kampuni za simu, taasisi za kifedha, wawekezaji na viongozi kufanya kazi kwa pamoja ili kuboresha mfumo wa ikolojia kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles