24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

SITA WAKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI

pembe za ndovu
pembe za ndovu

Na SAMWEL MWANGA-SIMIYU


POLISI mkoani Simiyu linawashikilia watu sita  wakazi wa Kijiji cha Mwabagimu wilayani Meatu kwa tuhuma ya kupatikana na nyara za Serikali, ikiwamo silaha na pembe za ndovu zenye uzito wa kilo 8 bila ya kuwa na kibali.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani  hapa, Onesmo Lyanga  alisema tukio hilo  lilitokea Januari 2, mwaka huu  saa 11 jioni kijiji humo.

Kamanda Lyanga ameitaja silaha hiyo  iliyokamatwa ni Rifle 375  yenye  namba  7054, pinde mbili zenye mishale 10 ambapo ina hisiwa miongoni mwa mishale  sita  imewekewa sumu kali ambayo inafanyiwa utaratibu kupelekwa kwa mkemia mkuu ili kubaini aina ya sumu na madhara yake.

Waliokamatwa ni Nghanga Ngusa (37), Machimu Ngusa (25), Mazongu Ngusa (22), Masasila Ngusa (20), Kulwa Ngusa (20) na Ntunga Shija (30) wote wakazi wa kijiji hicho.

Alisema kuwa siku ya tukio askari polisi wakiwa katika ulinzi wa kutekeleza amri ya baraza la ardhi chini ya usimamizi wa Mkaguzi wa Polisi, Frednand  Bundala kwa ajili ya kutoa ulinzi kwa dalali wa Mahakama, Abdalah Subira, ili kutekeleza amri ya baraza la ardhi na nyumba yenye namba 60/2016 ya kukabidhi ekari 70.

Alisema wakati wakisimamia zoezi hilo, ghafla  walipata upinzani mkubwa kutoka kwa watu walioamriwa kuondoka katika ardhi hiyo kwa kuwashambulia kwa mishale inayodhaniwa kuwa na sumu kali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles