24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Sita mbaroni kwa ubadhirifu wa sh. bil 1.6

Na Tunu Nassor -Dar es Salaam

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (TAKUKURU), Mkoa wa Ilala inawashikilia viongozi sita wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU Saccos) kwa ubadhilifu wa Sh bilioni 1.6.

Akizungungumza na waandishi wa habari leo Januari 10, 2020 Kamanda wa Takukuru mkoa wa Ilalal Christopher Myava amesema viongozi hao wanashikiliwa baada ya kubainika kutoa fedha kwa madai ya kuwakopesha wanachama 91.

Amesema hata hivyo walibaini kutokuwapo kwa  wanachama hao 91 na hivyo kusababisha upotevu wa fedha hizo.

“Tunafanya uchunguzi wa vyama vyote vya ushirika kwani tumebaini baadhi ya viongozi wamekuwa wakijinufaisha kwa kufanya ubadhirifu,” amesema Myava.

Amesema pia wanawashikilia watu watatu wa waliokuwa wakijifanya watumishi wa umma na uchunguzi dhidi ya makosa yao utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa.

Myava amesema katika kuhakikisha wanabaini mianya ya rushwa na kupata njia sahihi nya kuishauri Serikali, wamefanya uchambuzi wa mfumo wa matumizi fedha za ruzuku ya uendeshaji.

“Tumefanya uchambuzi wa mfumo wa uandikishaji wa vitambulisho vya taifa (NIDA)ili kubaini kama kunaweza kuwapo kwa mianya ya rushwa na kutoa ushauri kwa Serikali,” amesema Myava.

Amesema katika kipindi hicho cha miezi mitatu wamefanya ukaguzi na ufuatiliaji wa miradi yenye thamani ya Sh bilioni 13.5 inayotekelezwa na Serikali ukiwamo wa ujenzi wa machinjio ya Vingunguti.

mwisho  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles