30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Simu mpya yenye teknolojia ya AI yazinduliwa

Mwandishi Wetu

‘Simu janja’ mpya ya Infinix Zero 6, imezinduliwa rasmi ikiwa na teknolojia ya Artificial Intelligent (AI), yenye uwezo wa kupiga picha halisi ya mazingira husika kama bahari au picha zake huwa ni halisi zaidi na ikabaki katika ubora wake.

Ofisa Habari wa Kampuni ya Infinix, Aisha Karupa, amesema wadau wengi wameonesha kuguswa na simu hiyo ya kijanja kutokana na uwezo wake mkubwa tofauti na simu nyingine za mkononi.

“Ubora wa simu hii ambayo sasa inapatikana nchini, ni wa hali ya juu hasa upande wa kamera mbili za nyuma na mbili mbele, zenye uwezo mkubwa wa kupiga picha kutoka umbali mrefu.

“Pamoja na sifa nyingine za infinix Zero 6, sifa kuu zaidi ni kamera huku ikiwa imewekewa nguvu nyingi upande wa kamera ambapo kamera za nyuma ni zenye kupiga picha bora zenye mng’ao wa hali ya juu kama kamera ya mbele,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles