27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

SIMU INAVYOHARIBU AFYA YA MWANADAMU

Na JUSTIN DAMIAN


Je, umeshawahi kusoma kilichoandikwa kwenye kitabu cha maelezo juu ya namna ya kutumia simu yako pindi unaponunua mpya? Vitabu vyote vya maelekezo ya namna ya kutumia simu huelekeza watumiaji kusikiliza simu ikiwa mbali kidogo na sikio, lakini ni wangapi wanafuata maelekezo hayo muhimu?

Suala la usalama wa watumiaji wa simu za mkononi limekuwa ni gumzo sehemu mbalimbali duniani. Hata hivyo, kampuni kubwa za simu zimekuwa zikitumia mamilioni ya dola za Marekani kulinda biashara yao kwa kuhakikisha walaji hawapati ukweli wa madhara yanayotokana na simu.

Kwa kipindi kirefu, kumekuwapo madai kutoka kwa wanasayansi pamoja na vyombo vya habari kuwa matumizi makubwa ya simu za mkononi yanasababisha madhara kwa afya ya mtumiaji. Kwa miaka ya hivi karibuni, utumiji wa simu za mkononi umeongezeka mara dufu karibu kila kona ya dunia. Kwa sababu ugonjwa kama satarani unachukua miaka 10 hadi 20  kugundulika, pengine itachukua miaka mingi kwa watafiti kuihakikishia dunia kuwa matumizi ya simu yanasababisha saratani au hapana.

Mashirika ya kimataifa yamekuwa yakifanya utafiti kuhusu suala hili. Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani (IARC) ambalo ni sehemu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) liliwahi kuwaleta pamoja watengenezaji wa simu za mkononi ili kutoa data zinazohusiana na mionzi inayotokana na simu za mkononi.

Ilielezwa kuwa, simu hutoa mionzi inaitwa Radio Frequency-Electromagnetic Radiation (RF-EMR), ambayo pia hujulikana kama microwave radiation. IARC walisema kuwa mionzi hiyo inaweza kusababisha saratani. Hata hivyo, hakuna utafiti wa kina uliofanyika kuonyesha kama kweli simu za mkononi ni hatari au salama kiasi gani kwa watumiaji.

Kutokana na hilo, IARC ilitengeneza mradi uliokuwa unaitwa Interphone Project ambao ulijaribu kuchunguza madhara yanayotokana na matumizi ya simu za mkononi. Baada ya miaka 10, mradi huo ulimalizika Februari 2012, lakini wanasayansi walisema kuna ushawishi ulioingilia uchunguzi huo na hivyo hawakuweza kutoa uamuzi wa maana.

Katika hatua nyingine, Kituo cha Kuzuia na Kupambana na Magonjwa cha Marekani (CDC) mwaka 2014 kilitoa onyo kwa matumizi ya simu kwa kuwa swali la kuwa simu zinasababisha satarani au hapana bado halijapata jibu la uhakika. Hata hivyo, CDC waliondoa tangazo hilo kutoka kwenye tovuti yake kutokana na msukumo mkubwa kutoka kampuni ya simu. Kwa sasa CDC wanasema utafiti unahitajika kufanyika ili kujua matumizi ya simu yana madhara kiasi gani kwa watumiaji.

 

Watafiti wansema nini?

Mwaka 2007 na 2012 wanasayansi wa Uingereza walichapisha taarifa mbili zilizohuhusu madhara ya simu za mkononi na ubongo. Katika taarifa yao hiyo, walisema utafiti ulifanywa kwa mtu mmoja mmoja na kuonyesha madhara kwa watu waliokuwa wakitumia simu za mkononi.

Utafiti mwingine uliofanywa kwa wanyama umeweza kuonyesha uhusiano kati ya matumizi ya simu na madhara ya kiafya. Mwaka 2015 utafiti ulifanyika nchini Ujerumani ulionyesha uhusiano kati ya mionzi ya simu za mkononi na matatizo ya afya ya ubongo ya panya waliomtumia kufanya utafiti huo. Katika utafiti huo, watafiti hao pia waligundua kuwa mionzi inayotokana na simu za mkononi ni moja kati ya visababishi vya saratani. Pamoja na kwamba utafiti huu ulifanyika kwa panya lakini unaonyesha kuwa mionzi ya simu za mkononi inawenza kusababisha matatizo hata kwa binadamu.

Mwezi Mei mwaka 2016 utafiti mwingine wa miaka miwili ulifanyika nchini Marekani juu ya madhara ya mionzi ya simu kwa panya. Utafiti uligundua kwamba, panya waliokuwa kwenye mionzi ya wastani na mikali ya simu waliweza kupata madhara makubwa katika bongo zao. 

Japokuwa matokea ya tafiti ya juu ya madhara ya simu za mkononi kwa ubongo wa binadamu bado hazijatoa taarifa za uhakika sana, lakini watafiti wengi wamekuwa wakionyesha wasi wasi wao juu ya uhusiano wa afya ya ubungo na matumizi ya simu za mkononi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles